ALHAMISI 08/01/2015
Siku ya 2—Upendo
1 Yohana 4:7-21
Mapendekezo ya Huduma ya Maombezi:
Uwe huru kudai ahadi zingine pia. Kumbuka maagizo yote ya Mungu yana kuwezeshwa ndani yake!
Msifu Mungu kwa upendo wake usio na masharti.
Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. (1 Yoh. 4:19 )
Mwombe Mungu akupe upendo moyoni mwako kwa ajili ya waliopotea.
Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo
jema. Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshi
ma
mkiwatanguliza wenzenu. (War. 12:9, 10)
Hili ndilo pendo, si kwamba
sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma
Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda
sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. (1 Yoh. 4:10, 11)
Mwombe Mungu akupe upendo kwa jili ya adui zako na wale wanaokutesa.
Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.
Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. Wapenzi,
msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa,
Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Lakini, Adui yako
akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo,
utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali
uushinde ubaya kwa wema. (War. 12:17-21)
Lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi. (Math. 5:44)
Ombea upendo wa Mungu utimilike katika kanisa lake.
Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. (Wakol. 3:14)
Lakini, kwa ajili ya upendo nakusihi, kwa kuwa ni kama nilivyo, Paulo
mzee, na sasa mfungwa wa Kristo Yesu pia. Nakusihi kwa ajili ya mtoto
wangu niliyemzaa katika vifungo vyangu, yaani, Onesimo; ambaye zamani
alikuwa hakufai, bali sasa akufaa sana, wewe na mimi pia. (Wafilipi.
1:9-11)
Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana,
Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu. (1 Yoh.
4:12)
Ombea maisha yako na ya kanisa lako vioneshe upendo wa Mungu kwa wote wanaowazunguka.
Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo. (1 Kor. 16:14)
Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari;
haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu;
hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo
haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo
lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika. (1 Kor. 13:4-8)
Omba ili chochote kisikutenge na upendo wa Kristo. Mwombe Mungu
akuoneshe mambo yale yanayokutenga kutoka kwake, na uyasalimishe mambo
hayo kwa Mungu.
Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala
mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala
yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini,
wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu
ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu. (Warumi 8:38, 39)
Ombea
mahusiano ya upendo katika familia za Kiadventista. Ombea kwa namna ya
pekee familia zinazopitia migogoro ya ndoa au zinazokaribia kupeana
talaka. Je, unazijua baadhi ya familia hizo? Wainue kwenye maombi.
Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi. (1 Pet. 4:8)
Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo. (1 Kor. 16:14)
Na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha
kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi. (War.
5:5)
Ombea mahusiano ya upendo ndani ya Kanisa la Mungu.
Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. (1 Yoh. 4:7)
Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano
wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo. Kwa kuwa
mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile
isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. (1
Pet. 1:22, 23)
Ombea msisitizo wako binafsi na ule wa kikanisa
kuhusiana na mpango wa kila siku wa usomaji na kujifunza Biblia
ujulikanao kama Kuvuviwa na Neno Lake.
Kila andiko, lenye pumzi ya
Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa
kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe
kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. (2 Tim. 3:16, 17)
Unifumbue macho yangu niyatazame Maajabu yatokayo katika sheria yako. (Zab. 119:18)
Ombea ongezeko la mtazamo wa uharaka na utambuzi wa viongozi wa kanisa
na washiriki kuwa tunaishi katika nyakati za mwisho na kwamba Yesu yu
karibu kuja.
Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima. (Waef. 5:15, 16)
Ombea mahitaji binafsi ya mtu yeyote au lolote lililo moyoni mwako.
Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. (Wafil. 4:19)
Misheni kwenye majiji—Ombea Divisheni ya Euro-Asia na majiji
wanayoyafanyia kazi: Moscow, Urusi; Kiev, Ukraine; Kishinev, Moldova;
Donetsk, Ukraine; Kharkov, Ukraine; Minsk, Belarus; St. Petersburg,
Russia; Novosibirsk, Russia; Krasnoyarsk, East Russia; Khabarovsk,
Russia; Rostov-on-Don, Caucasus; Tbilisi, Georgia; Yerevan, Armenia; na
Almaty, Kazakhstan. Ombea shughuli maelfu za ushuhudiaji na matukio ya
uvunajai yanayoendelea hivi sasa.
Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, (Wakol. 3:23)
Msifu Mungu kwa mambo, hali, au watu ambao kupitia kwao unauona upendo wake kwako.
Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa
milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.” Niite, nami
nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. (Yer.
31:3)
Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali
kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa
dhambi zetu. (1 Yoh. 4:10)
Msifu Mungu kwa jibu lake lililotokana na ombi lako
Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika. (Ayu. 42:2)
Mwishoni mwa kipindi cha maombi, unaweza kuunda vikosi vya watu wawili
au watatu na kuwaombea watu saba ambao orodha yao utakuwa nayo mkononi.
Waombee ili wapokee upendo wa Mungu mioyoni mwao na wawapende wengine
kwa upendo wa kiungu. Dai 2 Wathesalonike 3:5 kwa ajili yao: “Sasa Bwana
mwenyewe na aiongoze mioyo yenu katika pendo la Mungu na subira ya
Kristo”
Kama una ombi la binafsi ambalo usingejisikia huru kuomba
kwenye kundi kubwa, jisikie huru kushiriki na mwenzako mmoja na
kuliombea.
Nyimbo zinazopendekezwa:
1. “I Love You Lord”; “Jesus Loves Me” (SDA Hymnal #190); “Anipenda Ni Kweli”; (Nyimbo za Kristo # 197)
2. “A Child of the King” (SDA Hymnal #468); “Baba Yetu Aliye Mbinguni” (Nyimbo za Kristo # 200) “
3. “Rescue the Perishing” (SDA Hymnal #367); Waponyeni Wtu” (Nyimbo za Kristo # 56)
4. “Lift High the Cross” (SDA Hymnal #362); “Msalaba wa Yesu” (Nyimbo za Kristo # 120)
5. “Seeking the Lost” (SDA Hymnal #373); “Kuwatafuta” (Nyimbo za Kristo # 200)
6. “I Will Sing of Jesus’ Love” (SDA Hymnal #183). “Niimbe Pendo Lake” (Nyimbo za Kristo # 31)
Ellen White kuhusu upendo
Lakini tunda la Roho ni upendo.—Gal. 5:22
Hapa pamewekwa jambo lenyewe ambalo tunatakiwa tulifanyie kazi: “Lakini
tunda la Roho ni upendo.” Ikiwa tuna upendo wa Kristo mioyoni mwetu
itakuwa ni sheria ya asili kwetu kupokea na zile neema zingine—furaha,
amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; “ na juu ya
mambo kama hayo hakuna sheria.” Sheria ya Mungu haimhukumu na kuwaweka
kwenye kifungo cha utumwa wale wenye neema hizi, kwa kuwa wanatii
matakwa ya sheria ya Mungu. Wao ni watunzaji wa sheria . . . hawapo
chini ya kongwa la utumwa wa sheria. . . .
Tunapaswa kuwa na
upendo, na vinavyoshikamana na jambo hili ni furaha, amani, uvumilivu,
utu wema. Tunaona kutotulia kwa dunia, hali yake isiyoridhisha. Watu
wanataka wasichokuwa nacho. Wanataka cha kuwasisimua au kuwaburudisha.
Lakini kwa Wakristo kuna furaha, kuna amani, kuna uvumilivu, kuna utu
wema, kuna fadhili, kuna uaminifu, na kuna upole; na kwa mambo haya
tunataka kufungua mlango wa moyo wetu, tukihifadhi neema za mbinguni za
Roho wa Mungu. . . . mmoja hawezi kulifanya hili kwa mwingine. Waweza
kutenda kazi na kupata neema za Roho, lakini hilo halitanipatia mimi
jibu. Kila mmoja ni lazima afanye kazi nay eye binafsi na kujiamulia
kupitia jitihada za binafsi kuwa na neema ya Mungu moyoni. Siwezi
kutengeneza tabia kwa ajili yako hata wewe huwezi kutengeneza tabia kwa
ajili yangu. Ni mzigo ambao unapaswa kuuelemea kila mmoja binafsi, awe
mdogo au mkubwa.
Kristo anasema: “Nitafanya wanadamu kuadimika
kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri. (Isaiah 13:12).
Kwa namna gani? Ulimaji wa neema za Roho—upendo, furaha, amani,
uvumilivu, utu wema, fadhili, na uaminifu. Tunataka imani iliyo hai
itakayokamata mkono wenye nguvu wa Jehova. . . . Sote tunahitaji neema
za Roho wa Mungu mioyoni mwetu.
Wakati pendo la Kristo
linapolindwa mioyoni mwetu, kama manukato mazuri haliwezi kufichika.
Mvuto wake mtakatifu unaoakisiwa kwenye tabia utadhihirika kwa wote.
Kristo ataumbika ndani, “tumaini la utukufu”When the (In Heavenly
Places, uk. 244).
Tunda la Roho ni upendo, furaha, na amani.
Migogoro na machafuko ni kazi za shetani na tunda la dhambi. Kama
tunataka kufurahia amani na upendo, ni lazima tuweke kando dhambi zetu;
ni lazima tuwe na muafaka na Mungu, na tuwe katika muafaka na wenzetu.
Hebu kila mmoja angejiuliza mwenyewe: Je, ninayo neema ya upendo? Je,
nimejifunza kuwa mvumilivu na kuwa na utu wema? Karama, kusoma, na uwezo
wa kuongea bila kuwa na hizi tabia za mbinguni itakuwa haina maana
yoyote sawa na shaba iliayo na upatu uvumao. Ni jambo la kusikistisha
kwamba hazina hii ya thamani inathaminiwa kidogo sana na inatafutwa
kidogo sana na wengi wanaojidai kuwa na imani! (Testimonies for the
Church, gombo. 5, uk. 169).
Popote roho inapounganika na Kristo,
kuna upendo. Chochote tabia itakachoweza kukimilika kitakuwa hakina
manaa kama hakina upendo, siyo upendo ule ulio mlaini, mdhaifu, na mteke
bali upendo ukaao ndani ya Kristo. Bila upendo, kila kitu hakina faida;
kwa kuwa hakiwezi kumwakilisha Kristo aliye upendo.” (Signs of the
Times, Dec. 28, 1891, par. 18).
Maswali ya kutafakari peke yako
1. Kuna mambo yoyote maishani mwako yanayokuzuia kumpenda Mungu kwa
moyo wako wote? Mwombe Mungu akuoneshe mambo hayo. Kisha mpatie mambo
hayo yote.
2. Je, kuna watu wowote maishani mwako ambao inakuwia
vigumu kuwapenda? Tumia muda fulani kumwomba Mungu akusaidie kuwa tayari
kuwapenda, akupe upendo moyoni mwako kwa jili yao na fursa ya
kuwaonyesha upendo wake (Mungu).
No comments:
Post a Comment