Pages

Saturday 17 January 2015

SIKU KUMI ZA MAOMBI ALHAMISI 15/01/2015

SIKU KUMI ZA MAOMBI
ALHAMISI 15/01/2015
Siku ya 9—Upole
Yakobo 3:13-18 & Wakolosai 3:12-17
Mapendekezo ya Huduma ya Maombezi:
Uwe huru kudai ahadi zingine pia. Kumbuka maagizo yote ya Mungu yana kuwezeshwa ndani yake!
Msifu Mungu kwa jinsi Yesu alivyoonesha mfano wa kuwa mpole.
Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake. (Isa. 53:7)
Msifu Mungu kwa kuwa anatuita tujifunze kwake na kwamba kwa kumuiga twaweza kuwa na amani.
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu. (Math. 11:29)
Msifu Mungu kwa kuwa upole wake unatufanya kuwa wakuu.

Nawe umenipa ngao ya wokovu wako, Mkono wako wa kuume umenitegemeza, Na unyenyekevu wako umenikuza. (Zab. 18:35)
Msifu Mungu kwa kuwa huwafundisha wapole njia yake.
Wenye upole atawaongoza katika hukumu, Wenye upole atawafundisha njia yake. (Zab. 25:9)
Mwombe Mungu akupe hekima yake yenye upole.
Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. (Yak. 3:17)
Mwombe Mungu akufundishe namna ya kuwa mpole.
Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole. (1 Tim. 6:11)
Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. (1 Pet. 3:3, 4)
Omba ili Mungu akufundishe namna ya kumrejesha kwa upole mtu aliye dhaifu na aliyeamguka.
Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. (Gal. 6:1)
Mwombe Bwana akufundishe kuwa mpole hata kwa wale wasio wapole kwako.
Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. (Filp. 4:5)
Kuna mtu yeyote au hali yoyote maishani mwako ambapo unahitaji kujifunza zaidi upole? Ombea hali hizo katika ukimwomba kujifunza kutoka kwake namna ya kuwa mpole.
Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu. (Zab. 18:32)
Mwombe Mungu akufundishe namna ya kujinyenyekesha.
Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake. (1 Peter 5:6)
Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa. (Math. 23:12)
Ombea uungawji mkono kukubwa na kuvutiwa kutoka kwa washiriki wa kanisa na viongozi kuhusu kudumisha elimu ya Waadventista wa Sabato ili ionekane kweli ni ya Kiadventista ya Kisabato katika maudhui na msisitizo. Hili ni la muhimu sana kwa mustakabali wa mtazamo wa nguvu kazi na utume.
Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee. (Mith. 22:6)
Ombea ongezeko la msisitizo wa vikun di vido vya ushuhudiaji, ili kwamba waumini wote washiriki katika ushuhudiaji binafsi na kutangaza ukweli mkuu wa Mungu katika siku hizi za mwisho.
Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. (1 Pet. 3:15)
Utume katika majiji—Ombea Divisheni ya Trans-European na majiji yake wanayojaribu kuyavuta kwa Yesu ya: London, Uingereza; Zagreb, Croatia; Tallinn, Estonia; Dublin, Ireland; Copenhagen, Denmark; Helsinki, Finland; Budapest, Hungary; Bergen, Norway; Randstad, Netherlands; Warsaw, Poland; Belgrade, Serbia; na Gothenburg, Sweden. Omba ili watu wawe na njaa kubwa ya Neno la Mungu.
Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Bwana. (Amos 8:11)
Ombea mahitaji yako yoyote ya binafsi au chochote kilicho moyoni mwako.
Nami ni maskini na mhitaji, Bwana atanitunza. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Mungu wangu, usikawie. (Zab. 40:17)
Msifu Mungu kwa kuwa hazuilii chochote kilicho chema kwa watoto wake na kwamba atakwenda kujibu maombi yako.
Kwa kuwa Bwana, Mungu, ni jua na ngao, Bwana atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu. (Zaburi 84:11)
. . . Wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! (Yak. 4:2b)
Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. (Yoh. 16:24)
Mwishoni mwa kipindi cha maombi, unaweza kuunda vikosi vya watu wawili au watatu na kuwaombea watu saba ambao orodha yao utakuwa nayo mkononi. Omba ili Mungu awafanye kuwa wapole na ili wawe washuhudiaji kwa ajili yake. Dai Yak. 1:19, 20 kwa ajili yao: “Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika; kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu.
Kama una ombi la binafsi ambalo usingejisikia huru kuomba kwenye kundi kubwa, jisikie huru kushiriki na mwenzako mmoja na kuliombea.
Nyimbo zinazopendekezwa
1. “I Love You Lord”; “Like Jesus”(SDA Hymnal #492); “Yesu Nakupenda” (Nyimbo za Kristo # 29)
2. “Take Time to Be Holy” (SDA Hymnal #500); “Tafuta DaimaUtakatifu” (Nyimbo za Kristo # 134)
3. “I Need the Prayers” (SDA Hymnal #505); “Nina Haja Nawe” (Nyimbo za Kristo # 126)
4. “Under His Wings” (SDA Hymnal #531). “Chini ya Msalaba” (Nyimbo za Kristo # 141)
Ellen White kuhusu Upole
Lakini tunda la Roho ni . . . Upole.—Gal. 5:23
Unatakiwa kumwakilisha Kristo katika unyenyekevu na upole na upendo. Upole wa kweli ni kito cha thamani machoni poa Mungu. (My Life Today, uk. 53).
Kama tuna Kristo akaaye ndani yetu, tutakuwa Wakristo nyumbani na nje pia. Yule aliye Mkristo atakuwa na maneno ya wema kwa kwa jamaa zake na watu watu anaoshirikiana nao. Atakuwa mwema, He will be kind, mwenye adabu, mwenye upendo, mwenye huruma, na atakuwa akijielimisha mwenyewe namna ya kuishi na familia ile iliyoko kule juu. Kama ni mwana familiya ya kifalme atauwakilisha ufalme anaokwenda kujiunga nao. Ataongea kwa upole kwa watoto wake, kwa kuwa atatambua wao pia ni warithi wa Mungu, wajumbe wa mabaraza ya mbinguni. Miongoni mwa watoto wa Mungu hakuna roho ya ujeuri ikaayo; kwa kuwa tunda la roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi: dhidi ya mambo hayo hakuna sheria. Roho ile inayopendelewa nyumbani, ndiyo roho itakayoonekana kanisani. (Ye Shall Receive Power, uk. 75).
Hakuna mwana familia anayeweza kujifungia mwenyewe mahali wana familia wenzake wasipoweza kuhisi mvuto wake. Mwonekano wa uvumilivu una mvuto wa wema au ubaya. Roho yake, maneno yake, matendo yake, hali yake inapoelekezwa kwa wengine, havifanyi makosa. . . . Kama amejazwa na upendo wa Kristo atadhihirisha adabu, wema, kujali hisia za wengine, na atawasiliana na wenzake, kwa njia ya matendo yake ya huruma, na hisia zake za kujali, zenye shukrani, na furaha. Itadhihirika wazi kuwa anaishi na Yesu. . . . Ataweza kusema kwa Bwana, “unyenyekevu wako umenikuza” (My Life Today, uk. 53).
Oh, ni lazima tuielimishe roho ili iwe yenye wema, ya kiungwana, inayojali, iliyojawa na msamaha, na yenye huruma. Wakati tukiweka kando majivuno, mazungumzo yote ya kipuuzi, vichekesho, na utani, hatupaswi kuwa baridi, tusiohurumia watu, na tusiochangamana na watu. Roho ya Bwana itatulia kwako hadi utakapofanana na ua lenye harufu nzuri lililochumwa kwenye bustani ya Mungu. Unatakiwa uendelee kuongelea nuru, ya Yesu, Jua la Haki, hadi utakapobadilika kutoka utukufu hadi utukufu, kutoka tabia hadi tabia, kutoka nguvu hadi nguvu, ukiakisi zaidi na zaidi sura nzuri ya Yesu. Utakapofanya hivi, Bwana ataandika kwenye vitabu vya mbinguni “Vema” kwa kuwa ulimwakilisha Yesu. (Ye Shall Receive Power, uk. 75).
Maswali ya kutafakari binafsi

1. Ni katika maeneo gani ya maisha unahitaji upole zaidi? Ni watu gani ungependa kuwaonesha upole zaidi?
2. Tengeneza orodha ya watu ambao ungeweza kuwa mpole zaidi kwao na umwombe Mungu akupe upole wake ili uuweze kumwakisi kwao. Msifu tangia mapema kwa ushindi anaokwenda kukupatia.
Siku ya 9—Upole Yakobo 3:13-18 & Wakolosai 3:12-17

No comments:

Post a Comment