Pages

Wednesday 14 January 2015

SIKU KUMI ZA MAOMBI JUMATANO 14/01/2015 Siku ya 8—Uaminifu Waebrania 11:1-11

SIKU KUMI ZA MAOMBI
JUMATANO 14/01/2015
Siku ya 8—Uaminifu
Waebrania 11:1-11
Mapendekezo ya Huduma ya Maombezi
Uwe huru kudai ahadi zingine pia. Kumbuka maagizo yote ya Mungu yana kuwezeshwa ndani yake!
Msifu Mungu kwa uaminifu na msamaha wake.
Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. (1 Yoh. 1:9)
Msifu Mungu kwa zawadi ya imani.
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha "...................ENDELEA HAPA........."
Mungu. (Waef. 2:8)
Msifu Mungu kwa kuwa habadiliki na hubaki mwaminifu hata wakati ule tunapokuwa si waaminifu.
Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe. (2 Tim. 2:13)
Msifu Mungu kwa kuwa hutuzawadia kwa uaminifu wetu.
Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele. (Mithali. 28:20a)
Ombea Mungu akufanye mwaminifu katika mambo madogo. Orodhesha baadhi ya mambo yale madogo ambayo unahitaji kujifunza kuwa mwaminifu kwayo.
Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia. (Luka 16:10)
Mwombe Mungu akupe imani na akusaidie kuamini.
Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. (Mark 9:23) Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii. (Luka 17:6 )
Mwombe Mungu akufundishe kutembea kwa imani na si kwa kuona.
Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona. (2 Kor. 5:7)
Omba ili usitumainie hekima ya kibinadamu bali uwezo wa Mungu.
Ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu. (1 Kor. 2:5)
Mwombe Mungu akuze imani yako.
Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani. (Luka 17:5)
Mwombee mchungaji wako wa mtaa, ukimwomba Mungu ampe mchungaji wako kipimo cha kutosha cha imani.
Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea. (Math. 21:22)
Ombea ili kila kiongozi wa kanisa ulimwenguni kote awe na mtazamo wa kina sana wa kiroho na wa kiuinjilisti. Msihi Bwana awalinde wachungaji na washiriki wa kanisa dhidi ya kupoteza utambulisho wa kiunabii unaotutambulisha kama kanisa la Waadventista wa Sabato, kanisa la Waliosalia la mwisho wa wakati.
Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema. (1Pet. 2:9, 10)
Ombea ongezeko la matumizi ya machapisho ya kikristo kwa washiriki wote wa kanisa na ongezeko la msisitizo wa uinjilisti wa vitabu ulio katika mfumo wa karatasi au wa kielektroniki.
Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. (2 Kor. 9:6)
Utume kwa majiji—Ombea Divisheni ya Southern-Asia Pacific na majiji ambayo wamejielekeza kushughulikia ya: Metro Manila, Philippines; Dhaka, Bangladesh; Cebu, Philippines; Makassar, Indonesia; Yangon, Myanmar; Urdaneta, Philippines; Karachi, Pakistan; Kota Kinabalo, Malaysia; Davao, Philippines; and Medan, Indonesia. Waombee wafanyakazi wajazwe na kupewa uwezo na Roho Mtakatifu.
Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. (Matendo 1:8)
Ombea hitaji lolote la binafsi au chochote kilicho moyoni mwako.
Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa. (Math. 7:7)
Msifu Mungu kwa kuwa mwaminifu katika kusikiliza na kujibu maombi yako. Msifu kwa yale anayokwenda kukutendea.
Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea. (Matt. 21:22)
Mwishoni mwa kipindi cha maombi, unaweza kuunda vikosi vya watu wawili au watatu na kuwaombea watu saba ambao orodha yao unayo mkononi. Waombee ili watafute amani ya Mungu mioyoni mwao. Dai Waebrania 11:6 kwa ajili yao: “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” Kama una ombi la binafsi ambalo usingejisikia huru kuomba kwenye kundi kubwa, jisikie huru kushiriki na mwenzako mmoja na kuliombea.
Nyimbo zinazopendekezwa
1. “Tis So Sweet to Trust in Jesus” (SDA Hymnal #524); “Kumtegemea Mwokozi” (Nyimbo za Kristo # 129)
2. “Standing on the Promises” (SDA Hymnal #518); “Yanipasa Kuwa Naye” (Nyimbo za Kristo # 154)
3. “My Faith Is Built on Nothing Less” (SDA Hymnal #522); “Cha Kutumaini Sina” (Nyimbo za Kristo # 69)
4. “It Is Well with My Soul” (SDA Hymnal #530). “Ni Salama Rohoni Mwangu” (Nyimbo za Kristo # 127)
Ellen White juu ya Imani na Uaminifu
Lakini tunda la Roho ni … uaminifu. (Gal. 5:22)
Ili kuja kwa Kristo, ni lazime pawepo zoezi la imani. Tunahitaji kumuingiza katika maisha yetu ya kila siku; ndipo tutakuwa na amani na furaha, na kujua kupitia uzoefu maana ya maneno yake, “Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.” (John 15:10).
Imani yetu ni lazima idai ahadi, kwamba tukae katika pendo la Yesu. Yesu alisema, “Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.” (fungu la 11).
Imani hutenda kazi kwa upendo nayo huitakasa roho. kupitia imani Roho Mtakatifu hutafuta namna ya kuufikia moyo, na kutengeneza utakatifu ndani yake. Mwanadamu hawezi kuwa wakala wa kutenda kazi za Kristo hadi amekuwa na umoja na Mungu kupitia Roho Mtakatifu. Tunaweza kufanywa tayari kwa ajili ya mbingu kupitia kubadilishwa kwa tabia pekee; Ni lazima tuwe na haki ya Kristo kama sifa au kigezo ikiwa tunataka kufika kwa Baba. Ni lazima tuwe warithi wa asili ya Mungu, tukiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. Ni lazima daima tubadilishwe kwa ushawishi wa Roho Mtakatifu; kwa kuwa ni kazi ya Roho Mtakatifu kuinua maonjo, kutakasa moyo, na kumboresha mwanadamu kwa kuwasilisha rohoni upendo usiokadirika wa Yesu. (Ye Shall Receive Power, p. 77).
Kila tendo la maisha, hata liwe dogo, lina mchango katika wema au ubaya. Uaminifu au kupuuzia yale yanayoonekana kama majukumu madogo kunaweza kufungulia mlango mibaraka mizuri maishani au maafa makubwa. Ni mambo madogo yanayopima tabia. Ni matendo ya kila siku yasiyo ya kujifanya na yenye kujikana nafsi, yaliyotendwa kwa moyo wa hiari, na uchangamfu, ambayo Mungu huyatolea tabasamu. Hatupaswi kuishi kwa ajili yetu wenyewe, bali kwa ajili yaw engine. Ni kwa njia ya kujisahahu wenyewe, kwa kuwa na moyo wa kupenda, na wa kusaidia wengine, ndipo twaweza kufanya maisha yetu kuwa mbaraka.
The little attentions, the small, simple courtesies, go far to make up the sum of life’s happiness, and the neglect of these constitutes no small share of human wretchedness (Conflict and Courage, p. 52).
Kwa kuwa mwaminifu katika kazi hii, siyo tu kunawasaidia wenzako, bali ndipo inapoamuliwa hatima ya maisha yako ya umilele. Kristo anatafuta kuwavuta wote watakaovutwa na mahusiano haya na yeye mwenyewe, kwamba tuwe na umoja naye, kwamba tuwe na umoja naye kama yeye alivyo umoja na Baba. Anaturuhusu kuchangamana na wanaoteseka na walio kwenye maafa ili atutoe kwenye uchoyo wetu; anatafuta kukuza ndani yetu tabia vipengele vya tabia yake—huruma, utu wema, na upendo. Kwa kuikubali kazi hii ya huduma, tunajiweka sisi wenyewe, kwenye shule yake, wakifanywa kuwa tayari kwa mabaraza ya Mungu. (Christ’s Object Lessons, p. 388).
Wale wanaoingia kazini kama “watumishi wapelelezi” watagundua kwamba kazi yao haitaweza kustahimili ukaguzi wa kidunia na wa malaika. Lililo la lazima ili kazi iweze kufanikiwa ni maarifa yanayomhusu Kristo; kwa kuwa ni maarifa haya yatakayoipa (kazi) kanuni sahihi na iliyo bora, na kuipa (kazi) roho bora na isiyo na ubinafsi kama ile ya mwokozi wetu tunayedai kumtumikia. Uaminifu, kubana matumizi, na kujali wengine, vitaonekana katika kazi zetu zote, popote tulipo, iwe ni jikoni, kwenye karakana, ofisini, hospitalini, chuoni, au popote tutakakopelekwa kikazi shambani mwa Bwana. “Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.” (Review and Herald, Sept. 22, 1891).
Tunapaswa kumwangalia Kristo, na kwa kumwangalia tunabadilishwa. Tunapaswa kuja kwake, kama kwa chemichemi isiyokauka iliyo kwa watu wote, ambayo kutokana nayo twaweza kunywa tena na tena na daima kukuta chemichemi ikiendelea kutoa maji safi. Tunapaswa kuitikia upendo wake unaotuvuta, kujilisha na Mkate wa Uzima ulioshuka chini kutoka mbinguni, kunywa Maji ya Uzima yanayobubujika kutoka kiti cha Enzi cha Mungu. Tunapswa kuendelea kuangalia juu, ili imani ituunganishe na kiti cha enzi cha Mungu. Usiangalie chini, kana kwamba umeunganishwa na dunia. Usiendelee kuipima imani yako, ukiing’oa, kana kwamba ni maua, ili uone kama yana mizizi. Imani hukua yenyewe bila kuonekana. (Ye Shall Receive Power, uk. 77).
Maswali binafsi ya kujadili
1. Una imani na Mungu hata katika mazingira magumu? Mwombe Mungu akuongezee! Dai Ahadi Zake.
2. Soma aya ya mwisho hapo juu. Orodhesha mambo unayoweza kufanya kuongeza imani yako. Mwombe Mungu akufundishe namna ya kuyatumia maishani mwako.

No comments:

Post a Comment