Pages

Thursday 8 January 2015

ALHAMISI 08/0102015 Siku ya 2—Upendo 1 Yohana 4:7-21

ALHAMISI 08/01/2015
Siku ya 2—Upendo
1 Yohana 4:7-21
Mapendekezo ya Huduma ya Maombezi:
Uwe huru kudai ahadi zingine pia. Kumbuka maagizo yote ya Mungu yana kuwezeshwa ndani yake!
Msifu Mungu kwa upendo wake usio na masharti.
Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. (1 Yoh. 4:19 )
Mwombe Mungu akupe upendo moyoni mwako kwa ajili ya waliopotea.
Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshi
ma mkiwatanguliza wenzenu. (War. 12:9, 10)
Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. (1 Yoh. 4:10, 11)

Mwombe Mungu akupe upendo kwa jili ya adui zako na wale wanaokutesa.
Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema. (War. 12:17-21)
Lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi. (Math. 5:44)
Ombea upendo wa Mungu utimilike katika kanisa lake.
Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. (Wakol. 3:14)
Lakini, kwa ajili ya upendo nakusihi, kwa kuwa ni kama nilivyo, Paulo mzee, na sasa mfungwa wa Kristo Yesu pia. Nakusihi kwa ajili ya mtoto wangu niliyemzaa katika vifungo vyangu, yaani, Onesimo; ambaye zamani alikuwa hakufai, bali sasa akufaa sana, wewe na mimi pia. (Wafilipi. 1:9-11)
Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu. (1 Yoh. 4:12)
Ombea maisha yako na ya kanisa lako vioneshe upendo wa Mungu kwa wote wanaowazunguka.
Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo. (1 Kor. 16:14)
Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika. (1 Kor. 13:4-8)
Omba ili chochote kisikutenge na upendo wa Kristo. Mwombe Mungu akuoneshe mambo yale yanayokutenga kutoka kwake, na uyasalimishe mambo hayo kwa Mungu.
Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu. (Warumi 8:38, 39)
Ombea mahusiano ya upendo katika familia za Kiadventista. Ombea kwa namna ya pekee familia zinazopitia migogoro ya ndoa au zinazokaribia kupeana talaka. Je, unazijua baadhi ya familia hizo? Wainue kwenye maombi.
Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi. (1 Pet. 4:8)
Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo. (1 Kor. 16:14)
Na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi. (War. 5:5)
Ombea mahusiano ya upendo ndani ya Kanisa la Mungu.
Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. (1 Yoh. 4:7)
Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo. Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. (1 Pet. 1:22, 23)
Ombea msisitizo wako binafsi na ule wa kikanisa kuhusiana na mpango wa kila siku wa usomaji na kujifunza Biblia ujulikanao kama Kuvuviwa na Neno Lake.
Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. (2 Tim. 3:16, 17)
Unifumbue macho yangu niyatazame Maajabu yatokayo katika sheria yako. (Zab. 119:18)
Ombea ongezeko la mtazamo wa uharaka na utambuzi wa viongozi wa kanisa na washiriki kuwa tunaishi katika nyakati za mwisho na kwamba Yesu yu karibu kuja.
Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima. (Waef. 5:15, 16)
Ombea mahitaji binafsi ya mtu yeyote au lolote lililo moyoni mwako.
Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. (Wafil. 4:19)
Misheni kwenye majiji—Ombea Divisheni ya Euro-Asia na majiji wanayoyafanyia kazi: Moscow, Urusi; Kiev, Ukraine; Kishinev, Moldova; Donetsk, Ukraine; Kharkov, Ukraine; Minsk, Belarus; St. Petersburg, Russia; Novosibirsk, Russia; Krasnoyarsk, East Russia; Khabarovsk, Russia; Rostov-on-Don, Caucasus; Tbilisi, Georgia; Yerevan, Armenia; na Almaty, Kazakhstan. Ombea shughuli maelfu za ushuhudiaji na matukio ya uvunajai yanayoendelea hivi sasa.
Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, (Wakol. 3:23)
Msifu Mungu kwa mambo, hali, au watu ambao kupitia kwao unauona upendo wake kwako.
Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.” Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. (Yer. 31:3)
Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. (1 Yoh. 4:10)
Msifu Mungu kwa jibu lake lililotokana na ombi lako
Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika. (Ayu. 42:2)
Mwishoni mwa kipindi cha maombi, unaweza kuunda vikosi vya watu wawili au watatu na kuwaombea watu saba ambao orodha yao utakuwa nayo mkononi. Waombee ili wapokee upendo wa Mungu mioyoni mwao na wawapende wengine kwa upendo wa kiungu. Dai 2 Wathesalonike 3:5 kwa ajili yao: “Sasa Bwana mwenyewe na aiongoze mioyo yenu katika pendo la Mungu na subira ya Kristo”
Kama una ombi la binafsi ambalo usingejisikia huru kuomba kwenye kundi kubwa, jisikie huru kushiriki na mwenzako mmoja na kuliombea.
Nyimbo zinazopendekezwa:
1. “I Love You Lord”; “Jesus Loves Me” (SDA Hymnal #190); “Anipenda Ni Kweli”; (Nyimbo za Kristo # 197)
2. “A Child of the King” (SDA Hymnal #468); “Baba Yetu Aliye Mbinguni” (Nyimbo za Kristo # 200) “
3. “Rescue the Perishing” (SDA Hymnal #367); Waponyeni Wtu” (Nyimbo za Kristo # 56)
4. “Lift High the Cross” (SDA Hymnal #362); “Msalaba wa Yesu” (Nyimbo za Kristo # 120)
5. “Seeking the Lost” (SDA Hymnal #373); “Kuwatafuta” (Nyimbo za Kristo # 200)
6. “I Will Sing of Jesus’ Love” (SDA Hymnal #183). “Niimbe Pendo Lake” (Nyimbo za Kristo # 31)
Ellen White kuhusu upendo
Lakini tunda la Roho ni upendo.—Gal. 5:22
Hapa pamewekwa jambo lenyewe ambalo tunatakiwa tulifanyie kazi: “Lakini tunda la Roho ni upendo.” Ikiwa tuna upendo wa Kristo mioyoni mwetu itakuwa ni sheria ya asili kwetu kupokea na zile neema zingine—furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; “ na juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.” Sheria ya Mungu haimhukumu na kuwaweka kwenye kifungo cha utumwa wale wenye neema hizi, kwa kuwa wanatii matakwa ya sheria ya Mungu. Wao ni watunzaji wa sheria . . . hawapo chini ya kongwa la utumwa wa sheria. . . .
Tunapaswa kuwa na upendo, na vinavyoshikamana na jambo hili ni furaha, amani, uvumilivu, utu wema. Tunaona kutotulia kwa dunia, hali yake isiyoridhisha. Watu wanataka wasichokuwa nacho. Wanataka cha kuwasisimua au kuwaburudisha. Lakini kwa Wakristo kuna furaha, kuna amani, kuna uvumilivu, kuna utu wema, kuna fadhili, kuna uaminifu, na kuna upole; na kwa mambo haya tunataka kufungua mlango wa moyo wetu, tukihifadhi neema za mbinguni za Roho wa Mungu. . . . mmoja hawezi kulifanya hili kwa mwingine. Waweza kutenda kazi na kupata neema za Roho, lakini hilo halitanipatia mimi jibu. Kila mmoja ni lazima afanye kazi nay eye binafsi na kujiamulia kupitia jitihada za binafsi kuwa na neema ya Mungu moyoni. Siwezi kutengeneza tabia kwa ajili yako hata wewe huwezi kutengeneza tabia kwa ajili yangu. Ni mzigo ambao unapaswa kuuelemea kila mmoja binafsi, awe mdogo au mkubwa.
Kristo anasema: “Nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri. (Isaiah 13:12). Kwa namna gani? Ulimaji wa neema za Roho—upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, na uaminifu. Tunataka imani iliyo hai itakayokamata mkono wenye nguvu wa Jehova. . . . Sote tunahitaji neema za Roho wa Mungu mioyoni mwetu.
Wakati pendo la Kristo linapolindwa mioyoni mwetu, kama manukato mazuri haliwezi kufichika. Mvuto wake mtakatifu unaoakisiwa kwenye tabia utadhihirika kwa wote. Kristo ataumbika ndani, “tumaini la utukufu”When the (In Heavenly Places, uk. 244).
Tunda la Roho ni upendo, furaha, na amani. Migogoro na machafuko ni kazi za shetani na tunda la dhambi. Kama tunataka kufurahia amani na upendo, ni lazima tuweke kando dhambi zetu; ni lazima tuwe na muafaka na Mungu, na tuwe katika muafaka na wenzetu. Hebu kila mmoja angejiuliza mwenyewe: Je, ninayo neema ya upendo? Je, nimejifunza kuwa mvumilivu na kuwa na utu wema? Karama, kusoma, na uwezo wa kuongea bila kuwa na hizi tabia za mbinguni itakuwa haina maana yoyote sawa na shaba iliayo na upatu uvumao. Ni jambo la kusikistisha kwamba hazina hii ya thamani inathaminiwa kidogo sana na inatafutwa kidogo sana na wengi wanaojidai kuwa na imani! (Testimonies for the Church, gombo. 5, uk. 169).
Popote roho inapounganika na Kristo, kuna upendo. Chochote tabia itakachoweza kukimilika kitakuwa hakina manaa kama hakina upendo, siyo upendo ule ulio mlaini, mdhaifu, na mteke bali upendo ukaao ndani ya Kristo. Bila upendo, kila kitu hakina faida; kwa kuwa hakiwezi kumwakilisha Kristo aliye upendo.” (Signs of the Times, Dec. 28, 1891, par. 18).
Maswali ya kutafakari peke yako
1. Kuna mambo yoyote maishani mwako yanayokuzuia kumpenda Mungu kwa moyo wako wote? Mwombe Mungu akuoneshe mambo hayo. Kisha mpatie mambo hayo yote.
2. Je, kuna watu wowote maishani mwako ambao inakuwia vigumu kuwapenda? Tumia muda fulani kumwomba Mungu akusaidie kuwa tayari kuwapenda, akupe upendo moyoni mwako kwa jili yao na fursa ya kuwaonyesha upendo wake (Mungu).

No comments:

Post a Comment