Pages

Thursday 8 January 2015

SIKU KUMI ZA MAOMBI ..Siku ya 1—Kukaa katika Kristo Yohana 15:1-17

Siku ya 1—Kukaa katika Kristo
Yohana 15:1-17
Mambo ya kuombea yanayopendekezwa
Jisikie huru kudai ahadi zingine pia. Kumbuka maagizo yote ya Mungu ni njia zake za kukuwezesha!
Msifu Mungu kwamba ni Kristo anayezaa tunda ndani yako.
Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. (Yohana 15:4)
Msifu Mungu kwa njia anazokufundisha kukaa ndani yake.
Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye; wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani. (Wakolosai 2:6,7).

Omba kwamba Mungu akufundishe namna ya kukaa ndani yake.
Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi.” (Zekaria 4:6). 
Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.” (Yohana 15:16) 
Omba Roho Mtakatifu wa Mungu amwagwe juu yako ili uzae tunda la Roho.
Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili… tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu. (Yoeli 2:28, 29) 
Mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu; mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha. (Wakol. 1:10, 11) 
Mwombe Mungu akusaidie kuelewa vizuri hitaji lako la kukaa ndani yake na kukupa tamaa ya kufanya hivyo.
Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. (Yohana 15:4) 
Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. (Warumi. 12:2)
Ombea familia na marafiki waone haja ya kujifunza namna ya kukaa ndani yake.
Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao; nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama. (Ezek. 11:19).
Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. (Rom. 8:5)  
Ombea umoja wa kanisa unaotokana na ukweli 
Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.” (Yohana 17:20, 21) Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja 1 Wakorintho. 1:10 
Ombea mkutano wa Kamati Kuu unaofanyika San Antonio, ombea wajumbe, na ombea maamuzi yale yatakayofanyika huko. Ombea ili wajumbe wawe ndani ya Kristo, na kwamba wawe wamejisalimisha kikamilifu kwake, na kwamba Roho Mtakatifu awaongoze katika kila uamuzi.
Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. (Yakobo 1:5)
Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu. (Wagalatia. 2:20) 
Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. (Yohana 14:16, 17) 
Ombea viongozi wa kanisa (mchungaji wako wa mtaa, wa Konferensi, wa Union, wa Divisheni, na wa Konferensi Kuu) ili wajazwe na Roho Mtakatifu na wakae ndani ya Kristo. 
Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. (Warumi 12:2)
Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo. (Waefeso 2:10)
Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu. (Wagalatia 2:20) 
Ombea msisitizo endelevu wa mada ya Uamsho na Matengenezo kwa washiriki, kwa Konferensi, kwa Union, kwa taasisi, kwa Divisheni, na kwa Konferensi Kuu. Kumbuka kuombea maombi ya mnyororo ya 777 kwa umwagaji wa mvua ya vuli ya Roho Mtakatifu.
Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu. (Yoeli 2:28, 29)
Ombea mavuno makubwa ya roho yatokanayo na mbegu zilizopandwa wakati wa Mradi wa Usambazaji wa kitabu cha Tumaini Kuu kwa njia zake mbalimbali.
Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. (2 Wakorintho 9:6) 
Ombea ili kila mshiriki awe na mzigo wa kuongoa roho na kutambua kuwa mbingu inatutaka sote tufuate hatua za Yesu katika kushiriki na wengine imani yetu huku tukitegemea uongozi wa Mungu.
Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake. (Mathayo 9:37, 38)
Utume katika Majiji—Ombea Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati na majiji waliyoyachagua kuyafanyia kazi: Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo; Dar-es-Salaam, Tanzania; Addis Ababa, Ethi-opia; Kampala, Uganda; Kananga, Kongo ya Magharibi; Lodwar, Kenya; Kigali, Rwanda; Lubumbashi, Kongo ya Mashariki; Goma, Kongo ya Kaskazini Mashariki; Magara, Burundi; na Juba, Sudani Kusini. Ombea ili ngome ya shetani ivunjwe na mahusiano na Kristo yaimarishwe. 
Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema! (Warumi 10:14, 15)
Ombea mahitaji yako yoyote au chochote kilichoko moyoni mwako.
Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. (Mithali 3:5, 6)
Msifu Mungu kwa njia mbalimbali ambazo Yesu alituwekea mfano wa namna kukaa ndani ya Mungu. 
Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno.” (Yohana 4:34)
Msifu Mungu kwa namna anavyokwenda kufanyia kazi na kujibu maombi yako.
Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. (Yohana 15:7)
Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo. (1 Wakorintho 15:57)
Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina. (Waefeso 3:20, 21) 
Mwisho wa maombi, unaweza kuunda vikosi vya watu wawili wawili au watatu watatu na kuwaombea watu saba mlionao kwenye orodha. Waombee ili kwamba wawe na uhusiano unaodumu na Yesu Kristo. Dai Yohana 14:23 kwa ajili yao: “Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. (Yohana 14:23) kama una ombi lako la binafsi usilojisikia vizuri kulitoa kwenye kundi kubwa, jisikia huru kumweleza unayeomba naye ili muliombee kwa pamoja.
Nyimbo zinazopendekezwa:
1. “Live Out Thy Life Within Me” (SDA Hymnal #316); “Uishi Ndani Yangu” (Nyimbo za Kristo # 147)
2. “I Need Thee Every Hour” (SDA Hymnal #483); “Nina Haja Nawe” (Nyimbo za Kristo # 126)
3. “Draw Me Nearer” (SDA Hymnal #306); “Univute Karibu” (Nyimbo za Kristo # 148)
4. “I Surrender All” (SDA Hymnal #309). “Yote Namtolea Yesu” (Nyimbo za Kristo # 122)
Ellen White kuhusiana na kukaa ndani ya Kristo 
“Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.” (Yohana 15:4, 5)
“Kaeni ndani yangu” ni maneno yenye umuhimu mkubwa sana. Kukaa ndani ya Kristo maana yake ni imani iliyo hai, ya dhati na inayoburudisha ifanyayo kazi kwa upendo na kuitakasa roho. Humaanisha upokeaji wa kudumu wa roho ya Kristo, maisha ya kujitoa kikamilifu kwa huduma yake. Muunganiko huu unapokuwapo, matendo mema yatatokea. Uhai wa mzabibu utajidhihirisha wenyewe kupitia matunda yenye harufu nzuri kwenye matawi. Mgao endelevu wa neema ya Kristo utakubariki na kukufanya mbaraka, hadi uweze kusema na Paulo, “Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu. (Galatians 2:20) (Our Father Cares, uk. 124).
Siyo mguso wa kawaida na kristo unaohitajika, bali ni kukaa pamoja naye. Alikuita ili ukae naye. Hapendekezi kwako mibaraka itakayodumu kwa muda kitambo na ambayo hupatikana mara chache kupitia kumtafuta Bwana kwa bidii na inayotoweka mara unapojihusisha na majukumu yako ya kawaida ya maisha. Kukaa kwako na Kristo hufanya kila wajibu wa lazima kuwa mwepesi, kwa kuwa anachukua uzito wa kila mzigo. Amekuandaa ili ukae naye. Hii ina maana unapaswa kuhisi kuwepo kwa Kristo, kwamba unaendelea kuwa na Kristo, na unaiona akili yako ikitiwa moyo na kuimarishwa…. Usisimame nje ya Kristo, kama wengi wajidaio kuwa wakristo wa leo wafanyavyo. Kukaa “ndani yangu na ndani yako” ni jambo linalowezekana kufanyika, na mwaliko usingetolewa kama lingekuwa ni jambo usiloweza kulifanya. Yesu Mwokozi wetu kwa kudumu anakuvuta kwa Roho wake Mtakatifu, akifanya kazi na akili yako ili ukae na Kristo…. Mibaraka anayoimwaga yote imeunganika na matendo yako wewe mwenyewe. Je, Kristo atamkataa mtu? “Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.” (Yohana 6:37). Akizungumza na kundi jingine alisema, “Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima.” (Yohana 5:40) (In Heavenly Places, uk. 55). 
“Bwana anahitaji wanaume na wanawake wanaobeba katika maisha ya kila siku, nuru ya mfano wa utauwa, wanaume na wanawake ambao maneno na matendo yao yanaonesha kuwa Kristo anakaa mioyoni, kwenye kufundisha, kwenye kuongoza, na kwenye kuelekeza. Anahitji wanaume na wanawake wa maombi, ambao kwa kumenyana mieleka wakiwa peke yao, hupokea ushindi dhidi ya nafsi, na kisha huondoka na kwenda kushiriki na wengine kile walichokipokea kutoka chanzo cha nguvu.” (To Be Like Jesus, uk. 262). 
“Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.”(Matthew 7:20), Mwokozi aliwaambia. Wafuasi wote wa kweli wa Kristo huzaa tunda la utukufu wake. Maisha yao hushuhudia kwamba kazi njema imeanzishwa ndani yao na Roho wa Mungu, na tunda lao linaelekea kwenye utakatifu. Maisha yao yameinuliwa na yapo safi. Matendo sahihi ni tunda lisilokosea la utauwa wa kweli, na wale wasiozaa tunda la namna hii wanadhihirisha kuwa hawana uzoefu katika mambo ya Mungu. Hawapo kwenye mzabibu. Yesu alisema, “Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.” (Yoh. 15:4, 5) (Counsels to Parents, Teachers, and Students, uk. 329).
Kama tawi linavyopaswa kukaa kwenye mzabibu ili kupokea virutubisho vya muhimu vinavyolisababisha kunawiri, ndivyo wale wampendao Mungu na kutunza maneno yake wanavyopaswa kukaa ndani ya pendo lake. Bila Yesu hatuwezi kushinda hata dhambi moja, au kushinda hata lile jaribu dogo kabisa. Wengi wanahitaji Roho wa Kristo na uweza wake ili kuangaza uelewa wao, kwa namna ile ile Bathomayo alivyohitaji kuona. “Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.” Wote ambao kiuhalisia ni wa Kristo watanufaika na uzoefu huu.
Baba huwapokea ndani ya yule mpendwa, na kuwafanya lengo la utunzaji wake wenye huruma, na upendo. Muunganiko huu na Kristo utakuwa na matokeo ya utakaso wa moyo, maisha ya kiungwana, na tabia isiyo na makosa. Tunda lililozaliwa kwenye mti wa Kikristo ni “upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, na kiasi.” (Testimonies for the Church, gombo la. 4, uk. 355). 
Maswali ya kutafakari peke yako
1. Ungependa Kristo akae ndani yako na wewe ndani yake kiasi gani? Mwombe Mungu akupe kwa namna ya pekee, hamu ya kukaa ndani yake.
2. Je, kuna jambo lolote ambalo laweza kumzuia Roho Mtakatifu asiyabadilishe maisha yako? Lilete jambo hilo kwa Mungu kwa njia ya maombi na kulisalimisha kwake.

No comments:

Post a Comment