Pages

Friday 9 January 2015

SOMO LA TATU ,SIKU YA TATU KATI YA ZILE KUMI ZA MAOMBI

SIKU KUMI ZA MAOMBI
IJUMAA 09/01/2015
Siku ya 3—Furaha
Habakuki 3:17-19 & Isaya 12
Mapendekezo ya Huduma ya Maombezi
Uwe huru kudai ahadi zingine pia. Kumbuka maagizo yote ya Mungu yana kuwezeshwa ndani yake!
Msifu Mungu kwa kuwa furaha ni tunda la haki.
Matumaini yao wenye haki yatakuwa furaha. (Mithali. 10:28a)
Msifu Mungu kwa furaha inayopatikana kwa uwepo wake na kwa kumfuata.
Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele. (Zab. 16:11)
Msifu Mungu kwa kuwa twaweza kufurahi hata pale tuwapo kwenye dhiki zetu, na kwamba uweza wa Kristo wakaa juu yetu.
Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. (2 Kor. 12:9)

Mwombe Mungu akupatie furaha moyoni mwako.
Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu. (Rum. 15:13)
Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. (1 Thes. 5:16-18)
Mwombee mtu fulani anayehitaji furaha ya Mungu moyoni mwake.
Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini! (Waf. 4:4)
Wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu. (Neh. 8:10b)
Omba ili Mungu akufundishe kufurahi katika dhiki. Kama una hali yoyote akilini mwako inayokusumbua ilete sasa mbele ya kiti chake cha enzi.
Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. (1 Pet. 4:13)
Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha. (Zab. 30:5b)
Waombee wale wanaoteseka, ukimwomba Mungu awape furaha mioyoni mwao.
Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake. (Zab. 126:6)
Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia. Kwa maana Wewe utambariki mwenye haki; Bwana, utamzungushia radhi kama ngao. (Zab. 5:11, 12)
Kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu. (War. 12:12)
Mwombee kijana mmoja kwenye kanisa lako ili apate furaha ya kumfuata Kristo. Wainue vijana wa kanisa lako kwa kuwataja kwenye maombi.
Jisifuni kwa jina lake takatifu, Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana! (Zab. 105:3)
Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Mungu. (Zab. 70:4)
Ombea kukubalika kwa moyo na kwa shukrani kwa maandiko ya Roho ya Unabii kama yatumikavyo leo. Omba ili kwamba viongozi wa kanisa na washiriki wawe wanasoma vitabu hivyo kwa utaratibu wa kudumu.
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana. (Yosh. 1:8)
Ombea ongezeko la msisitizo juu ya fundisho zuri la uumbaji wa Biblia—kwamba dunia yetu iliumbwa kwa siku sita halisi, kwa mfuatano wa siku kwa Neno la Bwana.
Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu. (Waebr. 11:1-3)
Utume kwenye Majiji—Ombea Divisheni ya Inter-European na majiji waliyochagua kuyafanyia kazi: Geneva, Switzerland; Prague, Jamhuri ya Czech; na Vienna, Austria. Iinue pia Unioni ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika na majiji 43 waliyopanga kuyaingia katika miaka minne hadi mitano ijayo. Waombee washiriki wa kanisa na viongozi wanaofanya kazi kwenye majiji haya.
Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. (1 Pet. 3:15)
Ombea hitaji lolote la binafsi au chochote kilicho moyoni mwako.
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. (Math. 6:33)
Msifu Mungu kwa kuwa tayari ana jibu kwa ombi lako.
Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia. (Isa. 65:24)
Mwishoni mwa kipindi cha maombi, unaweza kuunda vikosi vya watu wawili au watatu na kuwaombea watu saba ambao orodha yao utakuwa nayo mkononi. Waombee ili wawe na furaha ya Mungu mioyoni mwao. Dai Zaburi 40:16 kwa ajili yao. “Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Bwana.” Kama una ombi la binafsi ambalo usingejisikia huru kuomba kwenye kundi kubwa, jisikie huru kushiriki na mwenzako mmoja na kuliombea.
Nyimbo zinazopendekezwa:
1. “Blessed Assurance” (SDA Hymnal #462);/“Kuwa na Yesu” (Nyimbo za Kristo # 51)
2. “There Is Sunshine in My Soul Today” (SDA Hymnal #470);/“Ni salama Rohoni Mwangu” (Nyimbo za Kristo # 127)
3. “Joy By and By” (SDA Hymnal #430);/“Furaha Kwa Ulimwengu” (Nyimbo za Kristo # 166)
4. “I Shall See the King” (SDA Hymnal #426);/“Uso kwa Uso” (Nyimbo za Kristo # 175)
5. “Until Then” (SDA Hymnal #632)./“Pana mahali Pazuri Mno” (Nyimbo za Kristo # 180)
Ellen White kuhusiana na Furaha
Lakini tunda la roho ni … furaha.—Gal. 5:22
Wale wanaokaa ndani ya Yesu watakuwa na furaha, uchangamfu, na shangwe katika Mungu. Unyenyekevu uliotiishwa utajionesha kwenye sauti, kuheshimu mambo ya kiroho na ya umilele kutajionesha katika matendo, na nyimbo. Nyimbo za furaha, zitatoa mwangwi kwenye midomo; kwa kuwa limevuviwa kutoka kiti cha enzi cha Mungu. (Testimonies for the Church, gombo la. 4, uk. 625).
Furaha ya Kristo ni takatifu, yenye uchangamfu usioghoshiwa. Si misisimko mirahisi inayoongoza kwenye maneno matupu au wepesi wa tabia. Hapana, tunapaswa kuwa na furaha yake, na furaha yake kuu ilikuwa kuona watu wakitii ukweli … msihi Mungu ukimwambia, “Najitoa kikamilifu. Najitoa mwenyewe kwako.” Kisha uwe mwenye furaha. Neno li ndani yako, likitakasa na na kuosha tabia yako. Mungu hataki watoto wake kutembea wakiwa wenye nyuso za mashaka na huzuni. Anataka mwonekano wenye upendo wa tabia yake udhihirike katika kila mmoja wetu tulio washiriki wa tabia ya uungu; ili tuokolewe na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. . . Hatujaachwa kama kundi la mayatima eti kwa kuwa Yesu amekufa . . . Inawezekana kupata ushindi baada ya ushindi, na kuwa watu wenye furaha kuliko wote katika uso wa dunia.” (Our High Calling, uk. 148).
Kwa nini furaha yetu haijawa kamili—kukamilika, na kutopungukiwa na chochote? Tuna uhakika kuwa Yesu ni Mwokozi wetu, na kwamba twaweza kushiriki bila malipo yoyote utajiri aliotununulia. Twaweza kumwamini, tukijua kwamba atatupatia neema na uwezo way a kutenda kama navyotuamuru. Ametupatia kila uhakika kwamba atatimiza yale yote aliyotuahidi. Ni upendeleo wetu kutafuta daima furaha ya uwepo wake. Anatamani tuwe wachangamfu na tujazwe na sifa kwa jili ya jina lake. Anataka tubebe nuru katika mwonekano wetu na furaha mioyoni mwetu. Tuna tumaini lililo juu zaidi kuliko furaha yoyote ambayo ulimwengu waweza kuitoa; kwa nini sasa tusiwe na furaha? (Signs of the Times, Aug. 11, 1909, par. 4).
Hebu tukazane kuwaelimisha waumini kufurahi katika Bwana. Furaha ya kiroho ni matokeo ya imani iliyo hai. Watu wa Mungu wanatakiwa kuwa waliojawa na imani kamili na waliojazwa na Roho Mtakatifu. Ndipo atatukuzwa ndani yao.” (Bible Training School, April 1, 1905, par. 2).
Si kile kilicho kando yetu, bali ni kile kilicho ndani yetu; si kile tulichonacho, bali vile tulivyo, ndivyo vitufanyavyo kuwa wenye furaha ya kweli. Tunahitaji moto wa uchangamfu kwenye madhabahu ya mioyo yetu; ndipo tutaviona vitu vyote katika nuru ya furaha, ma uchangamfu. Twaweza kuwa na amani ya Kristo . . . Ikiwa tutakuwa watii, wenye kumtumainia Mungu, kama watoto katika hali isiyo na shaka atumainiavyo wazazi wake wa kidunia, tutakuwa na amani—si kama amani ile itolewayo na dunia, bali amani ile ambayo Yesu huitoa . . . Maisha, maisha haya, yana mng’ao mwingi ndani yake ikiwa tutakusanya maua na kuiacha miiba na michongoma peke yake.” (In Heavenly Places, p. 245).
Maswali ya kujadili peke yako.
1. Wewe ni mkristo mwenye furaha? Kama siyo, ni nini hukuondolea furaha? Chukua muda maalumu kusalimisha mambo hayo kwa Mungu kwa njia ya maombi. Dai ahadi zake za kukupatia furaha. Mwombe akupe moyo wenye furaha.
2. Fikiria mambo unayoweza kufanya kukusaidia kuwa mwenye furaha wakati wote. Jiandalie mpango mkakati na muulize Mungu akusaidie kuutumia maishani mwako.

No comments:

Post a Comment