Pages

Wednesday 6 January 2016

SIKU YA-1: ROHO MTAKATIFU- HITAJI LETU KUU


Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwawapa Roho Mtakatifu hao wamwombao? Luka 11:13
Mapendekezo ya Utaratibu Kipindi cha Maombi
Kusifu: (Takribani dakika 10)
• Anzeni kipindi kwa kumsifu Mungu: Jinsi alivyo; kwa upendo Wake; Hekima Yake, Utakatifu Wake n.k.
• Msifu Mungu kwamba atakufundisha jinsi ya kukaa ndani Yake.
• Msifu Mungu kwamba yuko zaidi ya tayari kukupatia zawadi kuu, Roho Mtakatifu.
Kuungama na Kudai ushindi dhidi ya dhambi (dakika 5)
• Muombe Mungu akuonyeshe dhambi unazohitaji kuungama moyoni, ukidai ushindi dhidi ya dhambi hizo.


• Muombe Mungu msamaha kwa kutokuthamini karama ya Roho Mtakatifu kama ambavyo ulipaswa, na muombe Yeye kukupatia njaa na kiu ya Roho Mtakatifu.
• Mshukuru Mungu kwamba anakusamehe kulingana na 1Yohana 1:9.
Sala na Maombezi (dakika 35)
• Muombe Mungu kufunua zaidi tabia Yake ili upate kumjua Yeye.
• Muombe Mungu akupe uhiari wa kujazwa na Roho Mtakatifu.
• Omba kwamba wanafamilia wenzako na marafiki waone hitaji lao la Roho Mtakatifu.
• Je kuna jambo lo lote linalomzuia Roho kuingia moyoni mwako? Mwambie Mungu juu ya jambo hilo.
• Waombee viongozi wa kanisa (mchungaji wako, wachungaji wa konferensi, unioni, divisheni na Makao Makuu ya Kanisa ulimwenguni) kuona hitaji la Roho Mtakatifu katika maisha yao.
• Omba kwa ajili ya umoja wa kanisa katika ukweli na Roho.
• Omba kwa ajili ya lengo linalokua na linaloendelea la “Uamsho na Matengenezo” kwa washiriki, konferensi, unioni, taasisi, divisheni na makao makuu ya Kanisa ulimwenguni. Tilia maanani mtazamo wa mtu binafsi katika “Uamsho na Matengenezo” kwako wewe, familia yako, kanisa lako na jamii yako. Omba ili kwamba watu washiriki katika mpango wa “Kuungana Katika Maombi” ili kuomba kwa ajili ya mvua ya masika ya Roho Mtakatifu na utimilifu wa kitabu cha Yoeli 2, Hosea 6 na Matendo 2.
• Ombea kila mshiriki kuwiwa na mzigo wa kuongoa roho na kutambua kwamba mbingu inamtaka kila mmoja kufuata kielelezo cha Kristo kwa kushiriki imani yake binafsi akiongozwa na Mungu.
• Omba juu ya mkazo zaidi wa ya usomaji wa Biblia kila siku kwa mtu binafsi na kwa kanisa kiulimwengu pamoja na kuifuata Biblia kupitia mpango wa “Amini Manabii Wake” ambao unahamasisha usomaji na kujifunza Biblia pamoja na Roho ya Unabii.
• Utume Katika Majiji – Ombea Divisheni ya West-Central Africa na miji wanayopanga kuifikia kwa ajili ya Kristo: Lagos, Douala, Calabar, Accra, Abuja, Lome. Pia omba kwa ajili ya Divisheni ya Kusini mwa Asia na miji wanayopanga kuifikia kwa ajili ya Kristo: Mumbai, Kochi, Bidar, New Delhi, Coimbatore, Surat, Imphal, Vijayawada. Omba ili Neno la Mungu liweze kuzaa matunda.
• Omba ili watu saba katika orodha yako au zaidi waone hitaji lao na kufungua mioyo yao kwa Roho Mtakatifu.
• Omba kwa ajili ya mahitaji binafsi uliyo nayo.
Shukrani
• Mshukuru Mungu kwa zawadi ya Roho Mtakatifu
• Mshukuru Mungu kwa namna ambayo Roho Mtakatifu amekuwa akifanya kazi katika moyo wako.
• Mshukuru Mungu kwa namna anavyoenda kuokoa roho kwa ajili ya ufalme Wake katika siku hizi kumi.
Mapendekezo ya Nyimbo
“Tawala Ndani Yangu” no 147, “Nina Haja Nawe” no.126, Univute Karibu” no 148, Nijaze Sasa no.40, Tubatize Upya no.189

ROHO MTAKATIFU- HITAJI LETU
Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona, bisheni, nanyi mtafunguliwa. Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Maani ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka? Au akimwomba yai, atampa nge? Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapata watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao? Luka 11:9-13
Ni nguvu ya Roho inayohitajika. Kwako na kwa kondoo wa Mungu zipo hisia za kujitosheleza nafsi ambazo zapaswa kuvunjwa. Roho wa Mungu ni nguvu inayoshawishi. Wakati hili litakapoelezwa katika kanisa, kutakuwa na badiliko linaloamuliwa katka ufanisi wao wa kiroho. Bwana Mungu yupo tayari kutoa, lakini wengi hatawambui hitaji lao la kupokea. Wao ni dhaifu, wakati wangeweza kuwa wenye nguvu, hawana nguvu ambapo wangeweza kuwa na nguvu kutokana na kupokea ufanisi kutoka kwa Roho Mtakatifu.Mwangaza wao ni hafifu, waamshe kutoka katika kujitosheleza kwao, hali ya kujihesabia haki.
Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki na hukumu. (Yohana 16:7,8)
Tunahitaji mvuto wa Roho Mtakatifu unaolainisha, unaotiisha, utakasao ili kuzifinyanga tabia zetu na kuleta kila wazo katika nyara ya Kristo. Ni Roho Mtakatifu ambaye anatuwezesha kushinda, na kutuongoza kukaa katika miguu ya Yesu, kama alivyofanya Mariamu, na kujifunza upole Wake na unyenyekevu wa moyo. Tunahitaji kutakaswa na Roho Mtakatifu kila saa iliyo katika siku, tusije tukanaswa na adui na kuhatarisha roho zetu.
Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari. (Yohana 16:13-15)
Uamsho wa ucha Mungu wa kweli katikati yetu ni hitaji lililo muhimu zaidi kupita yote.
Kuupata uamsho huu lapaswa liwe jukumu letu la kwanza.Lazima kuwa na bidii ya dhati ya kupata mbaraka wa Bwana, si kwa sababu Mungu hayuko tayari kutumwagia baraka Zake, lakini kwa sababu hatuko tayari kupokea mibaraka hiyo. Baba yetu wa mbinguni yuko tayari kuwapatia Roho Wake Mtakatifu wale wamwombao kuliko wazazi wa duniani walivyo tayari kuwapatia vipawa vyema watoto wao. Bali ni kazi yetu kwa kuungama, kujinyenyekeza, kutubu na kwa ombi la dhati kutimiza vigezo vya kupokea mibaraka hiyo ya Mungu. Uamsho unatakiwa kutegemewa pekee katika majibu ya maombi. Wakati ambapo watu wana njaa ya Roho Mtakatifu wa Mungu, hawawezi kukubali kuhubiriwa neno; lakini pale ambapo nguvu ya Roho Mtakatifu itakapoigusa mioyo yao, ndipo mahubiri yatakayotolewa hayatapita bure.Tukiongozwa na mafundisho ya Neno la Mungu, na kuvuviwa na Roho Mtakatifu katika zoezi la busara kamili, wale watakaohudhuria mikutano yetu watapata uzoefu wa pekee na watakaporudi nyumbani watakuwa wameandaliwa kuutendea kazi mvuto wenye afya.
Kushuka kwa Roho Mtakatifu juu ya kanisa kunaangaliwa kama uzoefu wa siku za mbeleni lakini ni fursa ya kanisa kuupata sasa.Tafuta uzoefu huo, Omba kwa ajili ya uzoefu huo na amini juu ya uzoefu huo.
Ni lazima tuupate na mbingu inasubiri kutupatia uzoefu huo.
Kristo aliahidi karama ya Roho Mtakatifu kwa kanisa Lake na ahadi hiyo ni ya kwetu vile vile kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa awali. Lakini kama ilivyo kwa ahadi nyingine yo yote, ahadi hii inatolewa kwa masharti. Wapo wengi wanaoamini na kukiri kudai ahadi ya Bwana, wanaongea juu ya Kristo na kuhusu Roho Mtakatifu, hata hivyo hawapati faida yo yote. Hawajisalimishi roho zao kuongozwa na kutawaliwa na mawakala wa kimbingu. Hatuwezi kumtumia Roho Mtakatifu, Roho Mtakatifu ndiye anayetutumia sisi. Kupitia kwa Roho, Mungu anafanya kazi ndani ya watu wake “katika kutaka kwao na kutenda kwao, kwa kulitimiza kusudi Lake jema.” Wafilipi 2:13. Lakini wengi hawatakubaliana na hili, wanataka kujitawala wenyewe. Ndiyo maana hawapokei zawadi hiyo kutoka mbinguni. Ni kwa wale tu wanaomsubiri Mungu kwa unyenyekevu, wale ambao wanatafuta uongozi Wake na neema Yake watakaopokea Roho Mtakatifu. Nguvu ya Mungu inasubiri hitaji lao na ukubali wao. Mbaraka huu ulioahidiwa, ukidaiwa kwa imani huleta mibaraka mingine pamoja nao.
Maswali ya Kujitathmini
1. Neno wamwombao (aiteo) lililotumiwa katika mwisho fungu la 13 katika Luka 11 lipo katika namna endelevu ya kuendelea kuomba. Kwa nini unafikiri Mungu alitumia aina hii ya neno?
2. Je kuna jambo lo lote linalokuzuia kumuomba Mungu kila siku kwa ajili ya Roho Mtakatifu kuja katika moyo wako na maisha yako? Je utasalimisha mambo hayo kwa Mungu leo?

No comments:

Post a Comment