Pages

Friday 9 January 2015

SOMO LA NNE KATI YA YALE KUMI YA SIKU KUMI ZA MAOMBI

SIKU KUMI ZA MAOMBI
JUMAMOSI 10/01/2015
Siku ya 4—Amani
Yohana 14:25-31 & Mathayo 6:25-34
Mapendekezo ya Huduma ya Maombezi
Uwe huru kudai ahadi zingine pia. Kumbuka maagizo yote ya Mungu yana kuwezeshwa ndani yake!
Bwana asifiwe kwamba tunaweza kupata amani kwa kutii sheria yake.
Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza. (Zaburi 119:165)
Bwana asifiwe kwamba aliumia kwa ajili yetu ili tuwe na amani.
Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. (Isa. 53:5)
Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atu
lete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa. (1 Petro 3:18)
Mwombe Mungu akupatie amani ipityo fahamu zetu.
Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. (Fil. 4:6, 7)
Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. (Yoh. 14:27)
Mwombe Mungu akufundishe kukaa ndani yake na katika amani yake.
Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini. (Isa. 26:3)
Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu. (War. 15:13)
Mwombe Mungu akufundishe namna ya kutafuta amani na Mungu na watu wengine.
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao. (Waeb. 12:14)
Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani. (Yak. 3:18) Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu. (Math. 5:9)
Mwombe Mungu akufundishe kumruhusu akupiganie na kukupatia amani yake katika mazingira magumu.
Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya. (Kut. 14:14)
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. (Matt.11:28-30)
Unawajua watu wowote wanaohitaji amani ya Mungu mioyoni mwao? Waombee.
Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema Bwana akurehemuye.” (Isa. 54:10)
Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli. (Yer. 33:6)
Unawajua watu wowote wanaopitia majaribu? Waombee, ukimwuliza Mungu awape amani.
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu. (Yoh. 16:33) Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha. (Kut. 33:14)
Waombee wale wanaoteseka kwa ajili ya Kristo, mkiomba kwamba amani ikae mioyoni mwao. Kama unawajua watu hao kwa majina, uwaombee.
Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima. (Isa. 32:17)
Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu (War. 5:1, 2)
Unawajua watu wowote wanaohitaji kuwa na amani na Mungu na watu wengine? Waombee.
Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. Amina. (War. 16:20) Iweni na amani ninyi kwa ninyi. (1 Wath. 5:13b)
Ombea ulinzi wa vijana wetu dhidi ya mivuto ya kidunia inayoendelea kukua. Waombee ili waweke mkazo wao katika Neno la Mungu na huduma kwa wengine. Mwombee kwa jina lake kijana unayefahamu kuwa anahitaji ulinzi wa Mungu.
Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi. (1 Tim. 4:12)
Utume kwenye majiji—Ombea Divisheni ya Inter-American na majiji wanayojaribu kuyaleta kwa Kristo: Mexico City, Mexico; Caracas, Venezuela; Bogatá, Colombia; Nassau, Bahamas; Belize City, Belize; Georgetown, Guyana; Cali, Colombia; Cayenne, French Guiana; Guatemala City, Guatemala; Quetzaltenango, Guatemala; Port-au-Prince, Haiti; Tegucigalpa, Honduras; Mérida, Mexico; Puerto Rico (visiwa vyote); Santiago de los Caballeros, Jamhuri ya Kidominika; na Maracaibo, Venezuela. Ombea kwamba waumini waweze kubuni mikakati ya kuyafikia majiji haya makubwa.
Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. (Yak. 1:5)
Ombea mahitaji yako binafsi na chochote kilichopo moyoni mwako.
Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani. (Isa. 43:18, 19)
Mtukuze Mungu kwa kuwa amekusikia na atafanya zaidi ya yale tuombayo au kufikiri.
Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina. (Eph. 3:20, 21)
Mwishoni mwa kipindi cha maombi, unaweza kuunda vikosi vya watu wawili au watatu na kuwaombea watu saba ambao orodha yao unayo mkononi. Waombee ili watafute amani ya Mungu mioyoni mwao. Dai 1 Petro 3:11 kwa ajili yao, “Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana.” Kama una ombi la binafsi ambalo usingejisikia huru kuomba kwenye kundi kubwa, jisikie huru kushiriki na mwenzako mmoja na kuliombea.
Nyimbo zinazopendekezwa:
1. “Have Thine Own Way, Lord” (SDA Hymnal #567); “Nasikia Sauti Yako” (Nyimbo za Kristo # 142)
2. “Be Still My Soul” (SDA Hymnal #461); “Moyo Wangu Amka Sasa” (Nyimbo za Kristo # 66)
3. “Wonderful Peace” (SDA Hymnal #466); “Nina Haja Nawe” (Nyimbo za Kristo # 126)
4. “Leaning on the Everlasting Arms” (SDA Hymnal #469); “Furaha Gani” (Nyimbo za Kristo # 43)
5. “Turn Your Eyes Upon Jesus” (SDA Hymnal #290). “Moyoni” (Nyimbo za Kristo # 211)

Ellen White kuhusiana na Amani
Lakini tunda la Roho ni … amani—Gal. 5:22
Bwana amekusudia kwamba kila roho inayotii neno lake itakuwa na furaha yake, amani yake, na nguvu yake endelevu ya ulinzi. Wanaume na wanawake hao wanavutwa karibu naye daima, siyo tu wakati ule wanapopiga magoti mbele yake katika maombi, bali hata wakati ule wanapoendelea na shughuli zao za maisha. Ameandaa kwa ajili yao mahali watakapokaa naye, ambapo maisha hutakaswa kutoka katika uchafu wote, na ukosefu wa upendo. Kupitia muunganiko huu usiovunjika na yeye hufanyika kuwa watendakazi pamoja naye katika maisha yao ya kazi. (My Life Today, uk. 51).
Wengine hawana amani wala utulivu; wapo katika hali ya kudumu ya kuwa na wasiwasi, na wanaruhusu tamaa na misisimko kutawala mioyo yao. Hawajui uzoefu wa amani na kustarehe katika Kristo ni jambo la namna gani. Ni kama meli isiyo na nanga, inayoendeshwa na upepo na kutupwa huko na huko. Lakini wale ambao akili zao zinatawaliwa na Roho Mtakatifu hutembea kwa unyenyekevu na kujidhili; kwa kuwa wanatembea kwenye njia moja na Yesu, na watatunzwa katika amani timilifu, wakati wale wasiotawaliwa na Roho Mtakatifu wanalinganishwa na bahari isiyotulia. (Ye Shall Receive Power, uk. 73).
Kuna wale wengine wanaotafuta daima hazina ya mbinguni, lakini hawasalimishi kikamilifu tabia zao zisizofaa. Hawaifii nafsi ili kusudi Kristo aishi ndani yao, na kwa sababu hiyo hawaipati ile hazina ya thamani… Hawafahamu kamwe nini maana ya kuwa na amani na muafaka moyoni; kwa kuwa bila kuisalimisha nafsi kikamilifu hakuwezi kuwepo pumziko, wala furaha. Wanakaribia kuwa wakristo lakini bado hawajawa wakristo, wanaonekana kukaribia ufalme wa mbinguni, lakini hawawezi kuingia pale. Kuwa karibu na kuokolewa maana yake ni kuwa karibu na kupotea kikamilifu… (In Heavenly Places, uk. 49).
Njia pekee ya kujipatia amani na furaha ni kuwa na muunganiko ulio hai nay eye aliyeyatoa maisha yake kwa ajili yetu, aaliyekufa ili tupate kuishi, na anayeishi ili aunganishe nguvu zake na juhudi za wale waliodhamiria kushinda. (In Heavenly Places, uk. 33).
Maneno hayawezi kuelezea amani na furaha alivyonavyo yeye anayeliamini neno lake. Majaribu hayamsumbui, wala matusi hayamyumbishi. Nafsi imesulibiwa. Siku kwa siku majukumu yake yanaweza kuwa mazito, majaribu yake yanaongezeka, dhiki zake kuwa nzito; lakini hayumbi; kwa sababu hupokea nguvu inayolingana na hitaji lake. (My Life Today, uk. 51).
Kuna amani katika kuamini, na furaha katika Roho Mtakatifu. Kuamini huleta amani, na kumtumaini Mungu huleta furaha. Amini, amini! Roho yangu inaniambia amini. Tulia katika Mungu. Ana uwezo wa kukutunzia kile ulichokiweka katika tumaini lake. Atakuvusha ukiwa zaidi ya mshindi kupitia yeye aliyekupenda. (The Faith I Live By, uk. 121).
Maswali ya kutafakari:
1. Unayo amani moyoni? Ni mambo gani yanayokuondolea amani? Tumia muda fulani ukiomba, na kusalimisha mambo hayo, na kudai ahadi za Mungu.
2. Je unaamini kile Mungu asemacho kwenye neno lake? Kutimiza ahadi zake na kukupatia amani katikati ya mazingira magumu? Omba ili Mungu akupatie amani yake wakati na dhiki na majaribu.

No comments:

Post a Comment