Pages

Saturday 17 January 2015

SIKU KUMI ZA MAOMBI IJUMAA 16/01/2015 Siku ya 10—Kiasi

SIKU KUMI ZA MAOMBI
IJUMAA 16/01/2015
Siku ya 10—Kiasi
Matthew 4:1-11
Mapendekezo ya Huduma ya Maombezi:
Uwe huru kudai ahadi zingine pia. Kumbuka maagizo yote ya Mungu yana kuwezeshwa ndani yake!..........................

Msifu Mungu kwa kuwa anakupa nguvu ya kuwa na kiasi. Msifu Mungu kwa njia alizokupatia kuweza kuwa na kiasi katika mazingira magumu.
Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu. (Zab. 18:32
Msifu Mungu kwa kuwa uweza wake umekufanya kutimilika katika mapungufu yako.
Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.
Msifu Mungu kwa kuwa ndiye akupaye uhiari na msaada wa kuwa na kiasi.
Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. (2 Cor. 2:14)
Mwombe Mungu akusaidie kuhiari kujitawala.
Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. (Rom. 12:1, 2)
Mwombe Mungu akusaidie kuchukia mambo ya dunia na akupe upendo kwa ajili yake yeye tu na si kwa ajili ya vitu vingine. Mweleze mambo yale unayotaka kujifunza kuyachukia.
Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele. (1 Yoh. 2:15-17)
Mwombe Mungu akukumbushe kila unapojaribiwa kwamba mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu.
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu. (1 Kor. 6:19, 20)
Mwombe Mungu akusaidie kutenda yote kwa utukufu wake.
Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu. (1 Kor. 10:31)
Mwombe Mungu akusaidie kuishi maisha yaliyofichwa ndani yake.
Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu. (Wag. 2:20)
Ombea muunganiko wa shughuli za uinjilisti na ushuhudiaji za wanaume, wanawake, na watoto wa kanisa la Waadventista wa Sabato kote ulimwenguni. Omba ili tuwe na nguvu za Roho Mtakatifu kadri tunavyojisalimisha kwenye uongozi wake maishani mwetu.
Lakini Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru. Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema Bwana. (Yer. 1:7, 8)
Omba ili Mungu awalete kwenye mstari wa mbele viongozi watauwa, wanaofundishika, na wanyenyekevu katika siku za usoni watakaotoa uongozi uliojkita kwa Kristo wakati kanisa lake likitimiza jukumu lililotoka mbinguni kwa ulimwengu.
Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. (1 Pet. 2:5)
Omba ili Kristo alete amani na upendo kwa kaya na familiya za Waadventista wa Sabato. Omba ili uwepo wake ufukuze manyanyaso na misongo kwa njia ya nguvu itakasayo ya haki yake.
Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. (Kol. 3:14, 15)
Utume katika Majiji—Ombea Divisheni ya Magharibi ya Kati ya Afrika na majiji wanayoyafanyia kazi ili kuyaleta kwa Kristo ya: Lagos, Nigeria; Douala, Cameroon; Calabar, Nigeria; Accra, Ghana; Abuja, Nigeria; na Lome, Togo. Omba ili watu waone hitaji lao juu ya Kristo na waanze kumuitia.
Kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. (Rum. 10:13)
Ombea jambo lolote la binafsi au chochote kilicho moyoni mwako.
Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. (Phil. 4:19)
Msifu Mungu kwa kuwa hakuna lililo gumu kwake na kwamba amesikia na kujibu maombi yako.
Kwa maana macho ya Bwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. (2 Nyak. 16:9a)
Mwishoni mwa kipindi cha maombi, unaweza kuunda vikosi vya watu wawili au watatu na kuwaombea watu saba ambao orodha yao utakuwa nayo mkononi. Omba ili waitendee miili yao kama hekalu la Roho Mtakatifu na ili waweze kujitawala. Dai 1 Kor. 10:13 kwa ajili yao: “Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.” Kama una ombi la binafsi ambalo usingejisikia huru kuomba kwenye kundi kubwa, jisikie huru kushiriki na mwenzako mmoja na kuliombea.
Nyimbo zinazopendekezwa:
1. “I Love You Lord”; “Jesus Loves Me” (SDA Hymnal #190); “Yesu Nakupenda” (Nyimbo za Kristo # 29)
2. “A Child of the King” (SDA Hymnal #468); “Vito vya Thamani” (Nyimbo za Kristo # 196)
3. “I Will Sing of Jesus’ Love” (SDA Hymnal #183); “Niimbe Pendo Lake” (Nyimbo za Kristo # 31)
4. “Stand Up! Stand Up for Jesus” (SDA Hymnal #618); “Piga Panda” (Nyimbo za Kristo # 64)
5. “Onward, Christian Soldiers!” (SDA Hymnal #612). (Nyimbo za Kristo # 65)
Ellen White on Self-Control
Tunda la Roho ni . . . Kiasi. Gal. 5: 23
Mungu anawataka watu wote waitoe miili yao kwake kama kafara iliyo hai na siyo miili iliyokufa au inayokufa, kafara ambayo kwa matendo yake yenyewe inajitia ugonjwa, ikijijaza na uchafu na maradhi. Mungu anahitaji mwili ulio hai. Mwili, anatuambia, ni hekalu la Roho Mtakatifu, makao ya Roho wake, na anahitaji wote wanaobeba taswira yake kutunza miili yao kwa kusudi la utumishi wake na utukufu wake. “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.” (1 Corinthians 6:19, 20). Ili kutimiza hili, katika wema wenu tieni maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa,
Ni wajibu wetu kujua namna ya kuutunza mwili katika hali bora zaidi ya kiafya, na wajibu mtakatifu kuishi kulingana na nuru ambayo Mungu kwa ukarimu wake mkuu ametupatia. Tukiifumbia macho nuru kwa kuhofu kuyaona makosa yetu, amabayo hatupo tayari kuachana nayo, dhambi yetu haipungui badala yake inaongezeka. Ikiwa nuru itazuiwa kuingia kwa upande mmoja, nuru hiyo itapuuziwa kwa upande mwingine. Ni dhambi pia kuvunja sheria za miili yetu, kama ilivyo dhambi kuvunja mojawapo ya Amri Kumi.
Hatuwezi kumpenda Bwana kwa miyo yetu yote, kwa akili zetu zote, kwa mioyo yetu yote, na kwa akili zetu zote, wakati tunapenda kula vitupendezavyo, na ladha zituvutiazo zaidi kuliko kumpenda Bwana. Daima tunapunguza nguvu zetu za kumtukuza Mungu, wakati anapohitaji nguvu zetu zote, na akili zetu zote. Kwa mazoea yetu mabaya tunapunguza uwezo wetu wa kuyashikilia maisha, na bado tunadai kuwa wafuasi wa Kristo, tunaojiandaa kuukamilisha mwili usioonja mauti. . . . (Ye Shall Receive Power, uk. 79).
Mapatano ya dhati na matakwa ya Biblia yatakuwa mbaraka, siyo kwa roho tu, bali kwa mwili pia. Tunda la Roho siyo upendo tu upendo, furaha, na amani lakini na kisi pia. Hatujatumwa kuuharibu mwili, kwa kuwa ni hekalu la Roho Mtakatifu. Kisa cha Danieli kinatuonesha kuwa kupitia kanuni za dini, vijana waweza kushinda tamaa za mwili na kubaki kuwa wakweli kwa matakwa ya Mungu, hata kama itawagharimu kafara kuu. Vipi kama wangeafikiana na wale maofisa wa kipagani, na wangekubali mbinyo uliotokana na mazingira, kwa kula na kunywa kama ilivyokuwa desturi ya Wababeli? Hatua hiyo moja ya makosa huenda ingewapelekea kwenye makosa mengine, hadi muunganiko wao na Mungu uwe umeachia; na hivyo kusombwa na majaribu. Lakini wakati akimshikilia Mungu kwa tumaini lisiloyumba, roho ya nguvu ya unabii ilikuja juu yake. Wakati akifundishwa na wanadamu juu ya majukumu ya baraza, alikuwa amefundishwa na Mungu kusoma miujiza ya wakati ujao. (Testimonies for the Church, gombo la. 4, uk. 570).
Jipime moyo wako kwa karibu sana, na katika maisha yako muige yule aliye mfano usio na makosa, na yote yatakuwa mazuri kwako. Hifadhi dhamira iliyo safi mbele za Mungu. Katika yote uyafanyayo litukuze jina lako. Jivue ubinafsi na upendo wa ubinafsi. (Testimonies for the Church, gombo. 2, uk. 71).
Maswali ya kutafakari peke yako
1. Ni katika maeneo gani maishani mwako unapohitaji zaidi kuwa na kiasi? Tengeneza orodha ya mambo hayo na uiwasilishe kwa Mungu. Dai ahadi zake za ushindi na umshukuru tangu mapema kwa ushindi anaokwenda kukupatia.
2. Unamfahamu mtu mwingine yeyote anayehitaji kuwa na kiasi (kujitawala) zaidi? Tumia muda kuomba na kudai ahadi za Mungu kwa mtu huyu pia.

No comments:

Post a Comment