Pages

Sunday 11 January 2015

SOMO LA SIKU YA TANO KATIKA ZILE SIKU KUMI ZA MAOMBI.....KARIBU

SIKU KUMI ZA MAOMBI
JUMAPILI 11/01/2015
Siku ya 5—Uvumilivu
Luka 23:26-43
Mapendekezo ya Huduma ya Maombezi
Uwe huru kudai ahadi zingine pia. Kumbuka maagizo yote ya Mungu yana kuwezeshwa ndani yake!
Msifu Mungu kwa kuwa ndiye atupatiaye uwezo wa kubadilika.
Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu,” asema Bwana wa majeshi. (Zek. 4:6b)
Msifu Mungu kwa namna anavyokuvumilia.
Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba. (2 Pet. 3:9)
Mwombe Mungu ili
asiwakatishe tamaa wale wanaomngojea.
Bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia. (Isa. 40:31)
Mwombe Mungu akusaidie kuvumilia.
Ukae kimya mbele za Bwana, Nawe umngojee kwa saburi; Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu afanyaye hila. Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, Usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya. (Zab. 37:7, 8)
Mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha. (Kol. 1:11)
Mwombe Mungu akufundishe namna ya kushinda ubaya kwa wema. Ombea hali yoyote maalumu unayohitaji kujifunza kuushinda ubaya kwa wema.
Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema. (Rum. 12:17-21)
Mwombe Mungu akusaidie kuona majaribu anayoruhusu kukujia kama njia ya kujifunza kuvumilia. Kama unapitia majaribu hayo, yaweke kwenye orodha yako na uyaombee.
Mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno. Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. (Yak. 1:2, 3)
Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana. (2 Kor. 4:16, 17)
Mwombe Mungu akukumbushe kuwaombea wale wanaokuudhi.
Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana. (Kol. 3:12, 13a)
Unawafahamu watu wowote wanaopitia majaribu? Omba ili Bwana awafundishe kuvumilia.
Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. (Rum. 8:28)
Ombea umoja katika kanisa la Waadventista wa Sabato kote ulimwenguni kuanzia makundini na kwenye makanisa, umoja unaotokana na kuliheshimu na kulithamini Neno la Mungu, maombi ya unyenyekevu, uwezo wa Roho Mtakatifu, kujali sera/michakato vinavyotambulika na kanisa, na kujikita kikamilifu katika utume wa kanisa. Ombea unyenyekevu maishani mwetu ili kwa pamoja tuweze kujisalimisha katika uongozi wa Mungu kwenye mchakato wa kufanya maamuzi yatakayodumisha umoja wa kanisa.
Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja. (1 Kor. 1:10)
Ombea umoja na ushirikiano wenye nguvu kati ya kanisa na huduma zinazotegemeza kwenye ushuhudiaji wa kiuinjilisti wa kanisa.
Tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri; wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia. (Waeb. 10:24, 25)
Ombea matumizi ya kila nyanja ya mitandao ya kijamii katika kushiriki na wengine ujumbe wa malaika watatu katika mtindo nzuri wenye ubunifu kwa ajili ya watu wenye shughuli nyingi tulionao leo.
Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. (Yoh. 15:5)
Utume kwenye Majiji—Ombea Divisheni ya Amerika ya Kaskazini kwa kadri wanavyojaribu kuyafikia majiji yafuatayo: New York City, New York; Calgary, Canada; Indianapolis, Indiana; St. Louis, Missouri; Seattle, Washington; San Francisco, California; Oakland, California; Tampa, Florida; and Oklahoma City, Oklahoma. Ombea pia Divisheni ya Kaskazini mwa Asia-Pacific na majiji wanayojaribu kuyafikia ya: Tokyo, Japan; Daegu, Korea; Daejon, Korea; Wuxi, China; na Ulaanbaatar, Mongolia. Ombea Roho wa Mungu atende kwa nguvu katika majiji haya.
Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi. (Zek. 4:6b)
Ombea hitaji lolote la binafsi au chochote kilicho moyoni mwako.
Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. (Waf. 4:19)
Msifu Mungu kwa kuwa ana njia maelfu za kutusaidia tusipouona hata mmoja na kwamba atajibu maombi yako.
Kwa kuwa Bwana, Mungu, ni jua na ngao, Bwana atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu. (Zab. 84:11)
Mwishoni mwa kipindi cha maombi, unaweza kuunda vikosi vya watu wawili au watatu na kuwaombea watu saba ambao orodha yao unayo mkononi. Omba ili Mungu awafundishe uvumilivu. Dai Wakolosai 1:11 kwa ajili yao: “Mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha…” Kama una ombi la binafsi ambalo usingejisikia huru kuomba kwenye kundi kubwa, jisikie huru sasa kushiriki na mwenzako mmoja na kuliombea.
Nyimbo zinazopendekezwa:
1. “Not I, but Christ” (SDA Hymnal #570); “Si Mimi Kristo” (Nyimbo za Kristo # 17)
2. “Pass Me Not, O Gentle Savior” (SDA Hymnal #569); “Usinipite Mwokozi” (Nyimbo za Kristo # 22)
3. “Give of Your Best to the Master” (SDA Hymnal #572); “Yote Namtolea Yesu” (Nyimbo za Kristo # 122)
4. “Blessed Assurance” (SDA Hymnal #462). “Kuwa Na Yesu” (Nyimbo za Kristo # 51)
Ellen White kuhusu Uvumilivu
Lakini tunda la Roho ni … uvumilivu—Gal. 5:22
Upendo ni sheria ya ufalme wa Kristo. Bwana anamwita kila mmoja kufikia viwango vya juu. Maisha ya watu wake yanatakiwa kudhihirisha upendo, unyenyekevu, na uvumilivu. Uvumilivu hubeba kitu fulani, ndiyo vitu vingi huku ukiwa hautafuti kulipiza kisasi kwa neno au kwa tendo.
“Uvumilivu” una subira na makosa; unastahimili. Ikiwa wewe u mvumilivu, hutawaweka kwa wengine yale unayodhani ni makosa ya ndugu zako. Utatafuta kuwasaidia na kuwaokoa, kwa sababu wamenunuliwa kwa damu ya Kristo. “Ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.” “Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.” Kuwa mvumilivu maana yake si kuwa katika hali ya majonzi na huzuni, na moyo wenye uchungu, bali ni kuwa kinyume kabisa cha hayo. (My Life Today, uk. 52).
Upendo wa Yesu unatakiwa uwemo maishani mwetu. Utakuwa na mvuto mlaini unaotiisha mioyoni mwetu na katika tabia zetu. Utatusukuma kuwasamehe ndugu zetu, hata kama wametuumiza. Upendo wa Yesu ni sharti utiririke miyoni mwetu kwa maneno ya kiungwana na matendo ya huruma kwa wengine. Tunda la kazi hizi njema litaning;inia kwenye kishada cha mzabibu wa tabia. “Tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi.” (Review and Herald, Nov. 16, 1886, aya ya. 10).
Jaribu kuishi na amani na watu wote, na hebu mazingira yanayoizunguka roho yako yawe matamu na yenye harufu nzuri. Mungu husikia kila neno la kipuuzi linalotamkwa. Kama utapambana dhidi ya asili ya ubinafsi ya kibinadamu, utasonga mbele kwa mafanikio makubwa katika kushinda mazoea ya kurithi na yale tuliyojizoezesha nayo yanayotufanya tukosee. Kwa subira, uvumilivu, na ustahimilivu utafanikisha mengi. Kumbuka kwamba, huwezi kunyanyasika na maneno yasiyo na busara ya mtu fulani, lakini pale unapojibu bila busara ndipo unapopoteza ushinda ambao ungtakiwa uupate. Uwe mwangalifu na maneno yako. Uvumilivu na ukarimu huonekana katika matendo na maneno ya wale waliozaliwa mara ya pili na ambao huishi maisha mapya katika Kristo. (My Life Today, uk. 52).
Maswali ya kutafakari peke yako
1. Unayo tabia ya kulipiza kisasi wakati mtu anapokukosea? Unajisikiaje wakati watu wanapokutendea vibaya? Mwombe Mungu akufundishe kuwa mvumilivu. Dai ahadi zake.
2. Kuna mtu yeyote maishani mwako anayekukanyaga kwa makusudi? Mwombe Mungu akupe uvumilivu, upendo, na msamaha kwa mtu huyo, na akusaidie kuwaonesha upendo wake.

No comments:

Post a Comment