Pages

Wednesday 14 January 2015

SIKU KUMI ZA MAOMBI JUMANNE 13/01/2015 Siku ya 7—Fadhili Warumi 12:9-21

SIKU KUMI ZA MAOMBI
JUMANNE 13/01/2015
Siku ya 7—Fadhili
Warumi 12:9-21
Mapendekezo ya Huduma ya Maombezi:
Uwe huru kudai ahadi zingine pia. Kumbuka maagizo yote ya Mungu yana kuwezeshwa ndani yake!
Msifu Mungu kwa wema wake kwako.
Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako Ulizowawekea wakuchao; Ulizowatendea wakukimbiliao Mbele ya wanadamu! Utawasitiri na fitina za watu Katika sitara ya kuwapo kwako; Utawaficha katika hema Na mashindano ya ndimi. (Zab. 31:19, 20)
Hakika wema na fadhili "............ENDELEA HAPA.............."
zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. (Zab. 23:6)
Msifu Mungu kwa kuwa mtu mwema hupata upendeleo kwa Bwana.
Mtu mwema atapata upendeleo kwa Bwana; Bali mtu wa hila atahukumiwa naye. (Mith. 12:2)
Msifu Mungu kwa mazingira maalumu yaliyokuwezesha kuona fadhili zake kwako.
Naamini ya kuwa nitauona wema wa Bwana Katika nchi ya walio hai. (Zab. 27:13)
Msifu Mungu kwa kuwa mambo yote hufanya kazi pamoja na wale wampendao.
Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. (War. 8:28)
Mwombe Mungu akupe hekima na uelewa ili uweze kufanya kila kitu katika unyenyekevu wa hekima.
N'nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima. (Yak. 3:13)
Mwombe Mungu akuoneshe namna ya kuwa mwema kwa wanafamilia wenzako.
Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio. (Gal. 6:9, 10)
Mwombe Mungu akusaidie kuonesha wema kwa wageni.
Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu. (Heb. 13:16)
Omba ili usichukulie kuwa mema unayoyapata yametokea kwa uwezo wako na kwamba Mungu akukumbushe kuwa kila kitu kinatoka kwake.
Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka. (Yak. 1:17)
Omba ili Bwana akufundishe kuona na kuthamini wema wake.
Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini. (Zab. 34:8)
Ombea ongezeko la usomaji wa vitabu vya Danieli na Ufunuo. Omba ili watu waelewe na kuhubiri huduma ya hema takatifu kama namna bora ya kuelezea wokovu. Ombea muono ulio wazi juu ya Kristo na kazi yake kwa ajili yetu wakati wa uhai wake hapa duniani, mauti yake msalabani, huduma yake anayoendelea nayo Patakatifu pa Patakatifu kule mbinguni kwa ajili yetu, na kuja kwake mara ya pili hivi karibuni.
Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli. (2 Tim. 2:15)
Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu. (Waeb. 8:1, 2)
Ombea ongezeko la ushiriki na kujitoa katika shughuli za ushuhudiaji wa kiuinjilisti kwa washiriki wote wa kanisa na taasisi na waendelee katika kuutegemeza utume unaoendelea kanisani.
Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni. (Math. 5:16)
Ombea uanzishwaji wa vituo maelfu vya mvuto hasa katika majiji makubwa kote ulimwenguni, na ombea ili vituo hivi vilete tofauti kubwa katika maisha ya watu wakati wakipitia uzoefu wa ukweli wa Mungu kupitia huduma za Kikristo.
Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni. (Math. 5:13-16)
Utume katika Majiji—Ombea Divisheni ya Southern Africa-Indian Ocean na majiji wanayojaribu kuyaleta kwa Yesu: Luanda, Angola; Antananarivo, Madagascar; Lilongwe, Malawi; Maputo, Msumbiji; Saurimo, Angola; Bloemfontein, Afrika ya Kusini; Lubango, Angola; Kitwe, Zambia; and Harare, Zimbabwe. Ombea pia Divisheni ya Kusini mwa Asia na majiji wanayojaribu kuyaleta kwa Yesu ya: Mumbai, Kochi, Bidar, New Delhi, Coimbatore, Surat, Imphal, na Vijayawada. Omba ili Neno la Mungu likazae tunda.
Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma. (Isa. 55:11)
Ombea hitaji lako lolote lile au chochote kilichopo moyoni mwako.
Nawe utajifurahisha kwa Bwana, Naye atakupa haja za moyo wako. (Zab. 37:4
Msifu Mungu kwa kuwa anafurahia kujibu maombi yako na kwamba anaenda kujibu maombi yako na atayajibu kwa wakati na kwa namna atakayoona inafaa.
Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. (Marko 11:24)
Mwishoni mwa kipindi cha maombi, unaweza kuunda vikosi vya watu wawili au watatu na kuwaombea watu saba ambao orodha yao utakuwa nayo mkononi. Waombee ili watamani wema wa Mungu na wautake uwe mioyoni mwao na ili uakisiwe kwa wengine. Dai Mathayo 12:35 kwa ajili yao: “Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.” Kama una ombi la binafsi ambalo usingejisikia huru kuomba kwenye kundi kubwa, jisikie huru kushiriki na mwenzako mmoja na kuliombea.
Nyimbo zinazopendekezwa:
1. “Jesus Loves Me” (SDA Hymnal #190); “Anipenda Ni Kweli” (Nyimbo za Kristo # 197)
2. “Day by Day” (SDA Hymnal #532); “Njiani Huniongoza” (Nyimbo za Kristo # 155)
3. “I Need Thee Every Hour” (SDA Hymnal #483); “Ninakuhitaji” (Nyimbo za Kristo # 16)
4. “Leaning on the Everlasting Arms” (SDA Hymnal #469). “Kumtegemea Mwokozi” (Nyimbo za Kristo # 129)
Ellen White kuhusu Fadhili
Bali tunda lo Roho ni. . . fadhili.—Wag. 5:22
Wema wa kweli unahesabiwa kule mbinguni kama ukuu wa kweli. Kuwepo kwa hisia za maadili huamua uthamani wa mtu. Mtu aweza kuwa na mali na elimu, na bado awe asiye na thamani, kwa kuwa moto unaounguza wa wema haujawashwa kwenye madhabahu ya moyo wake.
Wema ni matokeo ya nguvu ya kiungu inayobadilisha asili ya mwanadamu. Kwa kuamini katika Kristo, jamii iliyoanguka ikakombolewa yaweza kuipata imani hiyo itendayo kazi kwa upendo na kuitakasa roho na uchafu wote. Ndipo tabia inayofanana na Kristo hutokea: maana kwa kumwangalia Kristo wanadamu hubadilishwa na kufanana naye, kutoka utukufu hadi utukufu, kutoka tabia hadi tabia. Tunda bora huzalishwa. Huundika tabia ile inayofanana na ya Mungu, yenye uadilifu, iliyonyoka, na yenye wema wa kweli na kudhihirishwa kwa jamii yenye dhambi.
Bwana amemweka kila mwanadamu kwenye mtihani na kipimo. Anatamani kutuhakikisha na kutujaribu kuona kama tutakuwa wema na kutenda mema katika maisha haya, kuona kama aweza kutuamini kiasi cha kutupatia hazina za milele, na kutufanya watoto wa familiya ya kifalme, na watoto wa mfalme wa mbinguni.
Hakuna ukomo kwa mema uwezayo kufanya. Kama utalifanya Neno la Mungu kuwa kipimo cha maisha yako, na kuyatawala matendo yako kwa maagizo yake, ukiyafanya makusudi na juhudi zako zote wakati wa kutimiza majukumu yako ni mbaraka na si laana kwa wengine, mafanikio yataweka taji juu ya jitihada zako.
Umejiweka wewe mwenyewe katika muunganiko na Mungu; umekuwa njia ya kupitishia nuru kwa wengine. Umeheshimiwa kwa kuwa mtenda kazi pamoja na Yesu.; na hakuna heshima ya juu unayoweza kupokeakuliko mibaraka iliyobarikiwa itokayo midomoni mwa Mwokozi: “Vema, mtumwa mwema na mwaminifu” (My Life Today, uk. 54).
Maswali ya kutafakari peke yako
1. Ni katika njia zipi umeuona wema wa Mungu maishani mwako katika siku za hivi karibuni. Tumia muda fulani kumshukuru Mungu kwa yale aliyokutendea.
2. Utafanya nini kuakisi wema huo [uliotendewa] kwa wengine? Mwombe Mungu akuoneshe kile unachoweza kufanya na uwezo wa kuakisi wema huo kwa wengine.

No comments:

Post a Comment